Dawah Kiulimwengu -Kampeni

Waislamu wa Sri Lanka, Hakuna wa Kuwalilia!!

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

(Imetafsiriwa)

Vidonda vyenye kuchuruzika damu mwilini mwa Umma wa Kiislamu ni vingi na vinaongezeka kwa kukosekana kwa ngao ya ulinzi na mlezi Khalifah; mojawapo ni janga la Waislamu wa Sri Lanka. Sri Lanka, Kisiwa cha Ceylon, Serendib, au Kisiwa cha Rubies, kama Waarabu walivyokuwa wakikiita zamani, ni kisiwa kilichoko katika Bahari Hindi, kusini mwa India, na baadhi ya watu wanaweza kushangaa kwamba Uislamu ulikuwa umewasili Sri Lanka katika karne ya kwanza ya Hijria kupitia wafanyabiashara Waislamu waliofika katika eneo hilo na watu wake wakaingia katika Uislamu kwa sababu waliona tabia njema, muamala na uaminifu wa wafanyabiashara hao, na kile walichokisikia kutoka kwao kuhusu dini hii.

Waislamu wanaishi mashariki na katikati mwa Sri Lanka, haswa katika eneo la Kandy (katikati), na idadi ya Waislamu wa kisiwa hicho inakadiriwa kuwa asilimia 9.7 kulingana na sensa rasmi ya mwaka 2012, lakini asilimia hii inaweza kuwa imebadilika kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi yao tangu sensa hii ilipo fanywa. Idadi ya misikiti inakadiriwa kuwa 2000, imeenea katika miji na vijiji muhimu, na pia ina shule na taasisi za kibinafsi za Kiislamu, na duru zingine zinaonyesha kuwa wanakadiriwa kuwa ndicho kikundi chenye elimu zaidi nchini.

Waislamu wa Sri Lanka wameteseka kutokana na dola za kikoloni ambazo zimechukua kwa mfululizo kisiwa hiki; Ureno, Uholanzi na Uingereza, na walikabiliwa na changamoto kutoka kwa misheni za wamishonari waliosaidiwa na mamlaka za kikoloni za Uholanzi na Uingereza, na wameteseka na wanaendelea kuteseka na uhalifu wa Mabudha kama vile Waislamu wenzao wa Rohingya wanavyoteseka huko Myanmar. Kama matokeo ya chuki ya Mabudhi wa kipagani kwa Uislamu na Waislamu, na hofu yao ya kuongezeka kwa idadi ya Waislamu katika maeneo hayo, ambapo Waislamu wa Sri Lanka wametengwa, nyumba zao, maduka na misikiti kulengwa, na wanakabiliwa na mauaji na mateso, na wanazuiliwa kutekeleza matambiko na matendo yao ya ibada. Wamesumbuliwa sana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Watamil na Wasinhalese katika kipindi kati ya 1983 na 2009, ambapo harakati ya waasi wa Kitamil wakati huo iliwahamisha Waislamu zaidi ya elfu sabiini kutoka kaskazini mwa nchi, na mamia ya Waislamu waliuawa. Mnamo Machi 2006, Waislamu wanne waliuawa na wengine walijeruhiwa katika mlipuko wa guruneti la mkono lililotupwa na washambuliaji wasiojulikana kwenye msikiti katika mji wa Akarabato, kilomita 350 mashariki mwa mji mkuu Colombo, ambapo mamia ya watu walikuwa wakiswali. Mabudha pia walifanya mashambulizi makali dhidi ya msikiti mmoja katika moja ya vitongoji vya mji mkuu mnamo Agosti 2013, na kusababisha Waislamu kufunga msikiti na kuhamishia mahali pao pa ibada kwa msikiti wa zamani. Vurugu dhidi ya Waislamu zilianza tena mnamo Juni 2014, zikilenga maeneo mawili ya kitalii ya pwani ya Waislamu, nyuma yake walikuwa ni Mabudha, ambayo yalisababisha kuuawa kwa watu wanne na kuchomwa kwa mamia ya nyumba na maduka. Mnamo mwaka wa 2017, zaidi ya mashambulizi ishirini dhidi ya Waislamu yalitekelezwa kwa kipindi cha miezi miwili katika mkoa wa Gintota, kilomita 115 kusini mwa mji mkuu, pamoja na kuchomwa kwa kampuni zinazomilikiwa na Waislamu na kushambuliwa na mabomu ya petroli kwenye misikiti. Mwanzoni mwa Machi 2018, nyumba na maduka yanayomilikiwa na Waislamu wilayani Kandy ziliharibiwa, kufuatia mapigano kati ya Mabudha na Waislamu ambayo yalisababisha vifo na kusababisha viongozi kutangaza hali ya hatari. Matukio hayo yalizuka baada ya kundi la vijana wa Kiislamu kumshambulia dereva wa lori wa jamii ya Mabudha wa Sinhalese baada ya ajali ya barabarani, ambayo ilisababisha kifo chake katika eneo la Dijana, na kuuawa kwa kijana wa Kiislamu mnamo 7 Machi 2018 baada ya kuzidiwa na kuchoma nyumba katika eneo moja. Mnamo 15 Mei 2019, kundi linalopinga Waislamu nchini Sri Lanka lilichoma moto kiwanda kaskazini mwa mji mkuu Colombo, huku mauaji na mashambulizi dhidi ya Waislamu yakifanyika katika kipindi hicho hicho.

Leo, pamoja na uhalifu huu na mwengine, mamlaka za Sri Lanka, zikisukumwa na watawa wenye msimamo mkali wa Kibudha, wanatumia janga la virusi vya Korona kueneza hofu juu ya Uislamu, na baya zaidi, mashirika kadhaa mashuhuri ya habari na wazalendo walio karibu na serikali ya sasa wamewalaumu Waislamu kwa kuhusika kwa kuenea kwa virusi hivi nchini kama vile alivyofanya jirani yao, India, na juu ya hayo, mamlaka za Sri Lanka zimechoma moto miili ya Waislamu walioambukizwa na virusi vya Korona licha ya familia yao kukataa kufanya hivyo, lakini, ilithibitishwa kuwa baadhi ya wale waliowachoma hawakuambukizwa na virusi vya Korona na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu.

Mpaka lini vidonda hivi vitaendelea kuchuruzika damu mwilini mwa Ummah wa Kiislamu?! Je, hakuna yeyote katika Ummah na majeshi yake anaye weza kusonga mbele na kuwasaidia ndugu zetu na dada zetu nchini Sri Lanka na katika nchi zote nyengine za Waislamu?!

Ewe Mwenyezi Mungu, kwako Wewe tunakushtakia udhaifu wetu, na ukosefu wetu wa usaidizi na udhalilifu mbele ya watu, Ewe Mwenyezi Mungu, turuzuku Nusra Yako uliyotuahidi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bara’ah Manasrah