Jumla

Algeria na Sudan: Mapinduzi Yametekwa Nyara na Wamagharibi!

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mnamo Jumanne, 2 Aprili 2019, Abdulaziz Bouteflika alijiuzulu kama rais wa Algeria kutokana na shinikizo la maandamano makubwa yaliyo chochewa na kufeli kwa utawala wake kutatua matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanayoikumba nchi hiyo. Maandamano yalianza Ijumaa, 22 Februari 2019 na yanaendelea hadi sasa! Bouteflika aliingia madarakani mwaka 1999 kwa kuungwa mkono na jeshi ambalo lilikuwa limetoka kusambaratisha chama cha Islamic Salvation Front (FIS) ambacho kilikuwa kimeshinda uchaguzi wa 1990 na kilikuwa kina azma ya kusimamisha Serikali ya Kiislamu na kutekeleza Shari’ah. Utawala wa Bouteflika umeegemea mrengo wa Uingereza na unatumia sheria na sera za kisekula za kirasilimali kusimamia taifa. Abdelkader Bensalah, mwandani wa karibu wa Bouteflika na spika wa bunge upande wa juu alichukua madaraka Jumanne, 9 Aprili 2019 na kuwa rais wa muda! Bensalah alingia madarakani baada ya Mkuu wa Majeshi, Lt Gen Ahmed Salah, mwandani wa karibu wa Bouteflika aliposisitiza kupitia hotuba kwa ummah kuhusu kufanyiakazi kitengo 102 cha katiba ya Algeria kinacho ruhusu rais kuondoshwa mamlakani kwa misingi ya kuwa na hali mbaya ya kiafaya!

Mnamo Alhamisi, 11 Aprili 2019, Omar al-Bashir aliondoshwa mamlakani kama rais wa Sudan na baraza la kijeshi kutokana na shinikizo la maandamano makubwa yaliyo chochewa na hali ngumu ya maisha nchini humo. Maandamano yalianza Jumatano, 19 Disemba 2018 na yanaendelea hadi sasa! Omar al-Bashir aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Ijumaa, 30 Juni 1989. Utawala wa Omar al-Bashir umeegemea mrengo wa Marekani na unatumia sheria na sera za kisekula za kirasilimali kusimamia maisha ya watu. Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf, mwandani wa karibu wa Omar al-Bashir na Waziri wa Ulinzi alijitangaza kuwa ndiye Kiongozi pekee wa Serikali chini ya baraza la mpito la kijeshi mnamo Ijumaa, 12 Aprili 2019. Mnamo Jumamosi, 13 Aprili 2019, Awad alijiuzulu na kumtangaza Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, mwandani wa karibu wa Omar al-Bashir na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Miguu na hivi sasa ndiye Kiongozi wa pekee wa Serikali chini ya baraza la mpito la kijeshi!

Kwa mujibu wa maelezo hayo, masuala yafuatayo yamefichuliwa wazi:

Kwanza, raia wa nchi hizo mbili wanashiriki maandamano kutokana na kufeli kwa tawala hizo mbili katika kutatua maisha duni yanayoendelea kuwa magumu kila kukicha. Hivyo basi, hakuna mkono wa nje (mataifa ya nje) ambao ulichochea maandamano hayo ili kubadilisha utawala!

Pili, mataifa hayo mawili yana utajiri mkubwa unaoweza kutumika kuinua maisha ya watu lakini una uporwa na mabwana wakoloni wamagharibi, watala vibaraka na wandani wao huku wakiangamiza ustawi wa taifa! Kwa mfano, Algeria duniani ni nchi ya 10 inayozalisha gesi na ya 18 inayozalisha mafuta na Barani Afrika ni ya 1 inayozalisha gesi na ya 3 inayozalisha mafuta. Kwa upande mwingine, Sudan inazalisha mafuta na ina rasilimali nyingi za kilimo ambacho kinaajiri asilimia 80 ya waajiri na zinachangia kwa thuluthi moja ya uzalishaji jumla wa taifa (GDP). Kinaya ni kuwa bado tunashuhudia raia wa Algeria na Sudan wakifa maji wakikimbilia Ulaya eti kwa kutafuta “maisha mazuri!”

Tatu, nchi hizo mbili ziliongozwa na madikteta masekula wa koloni vibaraka kwa muda miongo mitatu ambao kibla chao ni London na Washington ili kupata muongozo wa namna ya kusimamia na kutekeleza sera za nyumbani na za kigeni. Zaidi ya hayo, la muhimu kwao ni kubakia kuwa watumwa watiifu kwa mabwana zao masekula warasilimali wakoloni kwa kuendeleza kukazanisha vitanzi vya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika shingo za raia wao!

Nne, viongozi wapya walioingia madarakani katika mapinduzi ya hivi karibuni si chochote bali ni muendelezo wa utawala muovu wa hali halisi na sera zao ambazo ahadi ya utiifu imebakia kwa mabwana zao wamagharibi. Kwa ushauri wa mabwana zao wamagharibi wamechukua madaraka kwa kubadilishana kupitia mlango wa nyuma kwa kudandia hisia za mapinduzi ya mabadiliko!

Kwa kuhitimisha, muhanga wa wanamapinduzi wahitaji kulindwa ili usije ukavunjiliwa mbali na kudandiwa na mbwa mwitu wamagharibi kwa jina la wapigiaji debe demokrasia. Ambao kiukweli ni wapigiaji debe kubakia kwa hali halisi na kuendeleza utelezaji wa mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazonuka zinazotokamana nazo ikijumuisha nidhamu ovu za kijamii ya kiliberali, demokrasia na uchumi wa kirasilimali miongoni mwa nyingine. Kinyume chake ni wanamapinduzi lazima wajifunze kutokana na hatima ya Mapinduzi ya Bara Arabu (Arab Spring) yaliyoanza mnamo 2011 nchini Tunisia na kusambaa hadi Misri, Libya, Yemen, Syria na miongoni mwa nchi za Mashariki ya Kati. Nchi nyingi zilibuni mabadiliko ya kisanii na kubadilisha watu au kuwapindua lakini masuala mawili muhimu yalibakia nidhamu ya utawala iliyotungwa na wanadamu na watawala vibaraka wa wakoloni wakiteleza nidhamu hiyo katika nyanja zote za maisha! Wafuatao waliondoshwa/waliuliwa: Hosni Mubarak (Misri), Ben Ali (Tunisia), Ali Abdallah Swaleh (Yemen), Muammar Gaddaffi (Libya) miongoni mwa wengine lakini maisha hivi sasa yamekuwa mabaya na yenye vurugu zaidi kuliko hapo awali!

Hivyo basi, hatua msingi na dharura kwa wanamapinduzi ili kulinda mapinduzi yao ni kulingania kurudi tena kwa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Kwa kuwalingania ndugu zao mukhlisina walio katika jeshi la Algeria na Sudan kutoa nusrah (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir. Ili kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah ikiongozwa na mtawala Khalifah anayetafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) pekee kwa kutumia Shari’ah (Qur’an na Sunnah) kusimamia mambo ya watu. Ni kupitia Khilafah pekee ndio Waislamu wataunganishwa kuwa Ummah Mmoja, Dola Moja chini ya Kiongozi Mmoja duniani kote pasina tofauti zao za lugha, ukabila au rangi. Khilafah itahakikisha kuwa hakuna raia Muislamu au asiyekuwa Muislamu (dhimmi) anapata maisha magumu kama inavyo shuhudiwa hivi sasa Algeria, Sudan na duniani kote kutokana na ulafi wa nidhamu za kirasilimali zinazoweka kipaombele maslahi ya mabwana wakoloni na watawala vibaraka na kuwafunga watu wote waliobakia katika utumwa wa kuendelea! Ni kupitia kusimamishwa kwa Khilafah ambapo amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kweli utakapo patikana. Chini ya Khilafah Uislamu na raia, na kwa ujumla matukufu, damu, mali na heshima zao zitalindwa.

Enyi, ndugu mukhlisina katika jeshi, Mwenyezi Mungu (swt) ana walingania mutoe nusrah:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. 

[Al-Anfal: 24]

Mweneyzi Mungu (swt) ana tukumbusha sisi:

(إِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ)

Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenya kufanikiwa.” [Al-Mujadila 58: 22]

 

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya