Jumla

Amani na Usalama wa Kweli Utadhaminiwa na Khilafah Pekee sio Serikali za Kisekula

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Kumeripotiwa kuwepo kwa wasiwasi mpya unaodhaniwa kutokana na polisi kuchukua hatua ya kuwaua washukiwa wa ugaidi badala ya kuwapeleka mahakamani baada ya Serikali kushindwa katika kesi za tuhuma za ugaidi mahakamani. Hii ni baada ya kufikia kikomo kwa kesi iliyoanza 6 Mei 2015 ya wanawake watatu wa Kiislamu kwa majina Ummulkheir Sadri, Khadija Abubakar na Halima Ali waliotuhumiwa kuwa wanachama wa Al Shabaab. Mahakama mjini Mombasa iliwaachilia huru watatu hao Alhamisi 11 Oktoba 2018 baada ya kukosekana ushahidi (The Standard Digital 14/10/2018). Uamuzi huo ulikuwa ni wa pili baada ya Haniya Sagar aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa tuhuma za ugaidi na hatimaye kukata rufaa na kuachiliwa huru kwa kukosekana ushahidi Ijumaa 5 Oktoba 2018 (The Standard Digital, 05/10/2018).

Tokea kwa kuvunjwa kwa Dola tukufu ya Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 Hijiria sawa na tarehe 3 March,1924, Ummah wa Kiislamu umebakia yatima aliyezongwa na madhila ya kila aina. Madhila haya yakiwa ni pamoja na kuvunjwa na kugawanywa kwa iliyokuwa Dola Moja yenye nguvu chini ya Khalifah mchaMungu aliyejifunga kikamilifu na Qur’an na Sunnah. Kinyume chake ikagawanywa na kuwa vijidola vilivyoasisiwa juu ya mipaka ya uzalendo na utaifa chini ya Ruwaiybidha (watawala wajinga) ambao wamejifunga na mfumo wa kisekula wa kirasilimali na daima wanaelekea Washington na London kama Qibla chao na twaa juu ya mabwana zao!

Marekani kama dola kubwa duniani na yenye kudhamini na kueneza mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali ulimwenguni kote. Inakwenda mbio kuhakikisha kuwa Waislamu hawajifungi na Uislamu wao kwa ukamilifu kwa maana kuwa hawaishi kwa kipimo cha Halali na Haramu bali wanaishi kwa kipimo cha maslahi/manufaa/madhara. Miongoni mwa hatua ilizochukua Marekani na washirika wake ni kutumia mwito wa ‘Kupambana na Ugaidi au Misimamo Mikali’ kama pazia ya kupambana na Uislamu na Waislamu popote walipo bora tu wawe wana mapenzi ya dhati juu ya Uislamu wao na wanafanya kazi usiku na mchana kulingania kurudi tena kwa ngao yao ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kampeni hiyo imepelekea kuwapa nguvu mpaka wale wanaojulikana kama waoga ulimwenguni ‘mayahudi’ eti nao kuwaotesha vidole na kuwatia hofu Waislamu kama inavyoshuhudiwa hivi leo yanayofanywa na umbile la Kiyahudi ndani ya Qibla cha Kwanza cha Al-Quds!

Kuanzia Mashariki hadi Magharibi na Kusini hadi Kaskazini kila serikali imenyoosha mikono yake kushirikiana na Marekani katika kampeni yake hiyo ovu na yenye maangamivu makubwa dhidi ya Ummah wa Kiislamu. Hivyo basi, Afrika haikuachwa nyuma kwa kuwa ni shamba la wakoloni wa Magharibi na Sera yake ya Kigeni inategemea mchoro wa Magharibi hususan Uingereza na Marekani. Japokuwa Uingereza na Marekani ni maadui wa kimaslahi barani Afrika  lakini uadui na chuki yao juu ya Uislamu na Waislamu iko wazi kwa kuwa wanautambua Uislamu kama mfumo pinzani na tishio dhidi ya mfumo wao batili.

Nchi za Afrika kwa kutegemea wa Magharibi na kiu isokwisha ya kupenda ‘misaada/pesa’ za kupambana na Ugaidi na Misimamo Mikali ikajitwika jukumu la kupambana kifikra dhidi ya Misimamo Mikali ndani ya mipaka yake na nje ya mipaka yake zikatuma majeshi eti kupambana na Ugaidi. Lakini kiuasilia Afrika ni bara lililopiga magoti na kujisalimisha mbele ya Marekani na washirika wake na kuwatumikia ipasavyo. Ikiwa ni pamoja na kuwateka nyara, kuwapoteza/ kuwaua na kuwafunga kidhulma raia (Waislamu) wa mataifa yao.

Marekani itasalimu amri hivi karibuni kama ilivyo salimu amri Dola ya Kifursi chini ya utawala wa Khalifah Umar ibn Khattab (ra) mwaka 651 Miladi. La msingi ni kuwa Amani na Usalama wa Kweli utadhaminiwa na Khilafah pekee sio dola hizi za Kisekula ambazo ndani ya majela yao kumejaa Waislamu kwa tuhuma za ugaidi na misimamo mikali.

Hivyo basi Waislamu popote walipo ni jukumu lao kujiunga na kufanya kazi yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ya kulingania kurudi tena kwa Khilafah kwa njia ya Utume. Kwani kupitia kwa Khilafah ndiyo Waislamu walioko nchini, China, Uturuki, Kenya Uzbekistan, Uganda, Afghanistan, Pakistan, Tanzania, Syria, Misr, Somalia n.k hawatotiwa uoga, korokoroni, kuuawa, kutekwa nyara n.k kama tunavyoshuhudiwa ulimwenguni kote. hivi leo. Kusimama kwa Khilafah kwa njia ya Utume kutahakikisha raia (Waislamu na wasiokuwa Waislamu) wake jumla watapata hifadhi na kusimamiwa mambo yao kwa ukamilifu na hatima yake ni kupatikana utulivu na ustawi.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya