Habari na Maoni

Angela Merkel anahofia Khilafah

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Habari na Maoni

 Habari:

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel aliwahi kusema; ‘Wajerumani wameshindwa kutambua jinsi uhamiaji wa Waislamu nchini kwao umebadilisha nchi yao na utafika wakati ambao Ujerumani itakua na misikiti mingi kuliko makanisa.’

“Nchi yetu itaendelea kubadilika,  …..kuamiliana…. pia ni kazi kubwa kwa jamii itakayo kumbana na jukumu hili,” Merkel aliliambia gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung Daily.

“Kwa miaka sasa tumekuwa tukijidanganya wenyewe kuhusu jambo hili. Wingi wa misikiti, kwa mfano itakua jambo la kawaida mijini mwetu zaidi ya ilivyokuwa hapo awali, Merkel aliongezea.

Ujerumani ina wingi wa waislamu wapatao milioni nne hadi milioni tano, huku kasi yao ya kuzaana ikiwa juu zaidi. Tamshi hili la Merkel ndilo tamshi la kwanza rasmi linalokubali wazi kuwa Ujerumani, sawa na nchi zenginezo Uropa, inakusudiwa kuwa ngome kuu ya Uislamu siku za usoni.

Nchini Ufaransa, asilli mia 30 (30%) ya watoto walio na miaka 20 kurudi chini ni waislamu. Asili mia ya watoto hawa mjini Paris na Marseille imeongezeka hadi asili mia 45 (45%). Ufaransa kaskazini, kuna misikiti mingi kuliko makanisa.

Nchini Uingereza, wingi wa Waislamu umeongezeka kutoka elfu 82 hadi milioni 2 unusu kwa mda wa miaka 30 iliyopita. Kwa sasa, kuna misikiti zaidi ya 1,000 nchini Uingereza, mingi yao ilikuwa makanisa hapo awali kabla ya kubadilishwa kuwa misikiti.

Nchini Ubelgiji, asili mia 50 (50%) ya watoto wanaozaliwa ni Waislamu na yasemekana kuwa wingi wa Waislamu nchini humo ni takriban asili mia 25 (25%)-takwimu sawiya na zile za Uholanzi. Hali ni hii hii nchini Urusi ambako mmoja kati ya wakaazi watano ni Muislamu.

Muammar Gaddafi wakati fulani alisema: “Kuna dalili kuwa Allah ataupa Uislamu ushindi bara Uropa bila ya upanga, bila ya bunduki, bila ya utekaji wa mataifa. Hatuitaji magaidi; hatuitaji walipuaji wa miji. Waislamu hawa milioni 50 na zaidi walioko Uropa wataigeuza Uropa kuwa bara la uislamu kwa mda wa miongo michache ijayo.”

Takwimu hizi zamuunga mkono.

Maoni:                    

Si wingi wa watu unaofanya nchi kuwa ya kiislamu  bali ni utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu kikamilifu[asili mia mia moja (100%)], kwa nchi ya Waislamu.

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel ywaipulizia sumu ya kulala ili kuilaza zaidi jamii ya kiislamu ambayo tayari imo usingizini yang’orota, wakati ni sasa wa jamii kuamka!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ ]

Enyi mlioamini Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume wake anapokuiteni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri]

[Anfal:24]

Makusudio makuu ya Merkel ni kuudunisha Uislamu kuwa ni dini ya kiroho tu  ambayo ibada zake zaanzia na kuishia(kukoma) misikitini. Lengo hili ni kinyume kabisa na Uislamu ambao kiuhalisia wake ni mfumo kamili unaogusa kila nyanja ya maisha: kijamii, kiuchumi, na kisiasa. Chansela huyu wa Ujeramani ywawaigiza wenzake wa Marekani, Donald Trump na George Bush mdogo ambao wakati fulani walisema kuwa Uislamu ni dini ya kiroho ya amani inayofuatwa na mamiliomi ya waislamu duniani kwote.

Kwa kusikiliza maneno bila makini, mtu anaweza kudhania kuwa viongozi hao wana mapenzi na Uislamu au hawana shida na Uislamu lakini lo! sivyo, bali ni kinyume chake; ni ufisadi (fitina) wanaeneza kwa kutia sumu akilini mwa jamii na kwa kufisadisha akili ya jamii.

[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

Wanataka kuizima nuru ya MwenyeziMungu kwa vinywa vyao na MwenyeziMungu amekataa ispokuwa kuitimizma nuru yake japokuwa makafiri wanachukia.

[Tauba:32]

Maskini wanajidanganya tu wenyewe, Nuru ya Allah si mwangaza wa mshumaa ili wapate kuizima kwa ndimi zao ama pumzi zao basi-ni Nuru ya uongofu.

[ هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ 

Yeye ndiye Aliyemleta Mtume Wake kwa uongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda dini zote  ijapokuwa watachukia hao washirikina.

[Tauba: 33]

Si kibahati kwamba viongozi hawa wapotoshaji wa dunia wanasoma kutoka kurasa ile ile moja ya ‘dini ya kiroho’, bali ni njama wanazofanya kwa ufahamu wanapokuwa wamealikana mezani katika sherehe zao za ‘Mwangaza wa Mshumaa’-wanakopanga mbinu zile bora za kuwatafuna waislamu na kunywa damu zao(waislamu); na ndio maana haistaajabishi kuwa dunia imetanda uchafu(uovu) mwingi zaidi

عَنْ ثَوْبَانَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏”‏ يُوشِكُ الأُمَمُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمْ كَمَا تَدَاعَى الأَكَلَةُ إِلَى قَصْعَتِهَا ‏”‏ ‏.‏ فَقَالَ قَائِلٌ وَمِنْ قِلَّةٍ نَحْنُ يَوْمَئِذٍ قَالَ ‏”‏ بَلْ أَنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيرٌ وَلَكِنَّكُمْ غُثَاءٌ كَغُثَاءِ السَّيْلِ وَلَيَنْزِعَنَّ اللَّهُ مِنْ صُدُورِ عَدُوِّكُمُ الْمَهَابَةَ مِنْكُمْ وَلَيَقْذِفَنَّ اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمُ الْوَهَنَ ‏”‏ ‏.‏ فَقَالَ قَائِلٌ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا الْوَهَنُ قَالَ ‏”‏ حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ الْمَوْتِ ‏”‏ ‏

Amepokea Thauban kwamba Mtume Saw Alisema: Mataifa yanakaribia kuitana dhidi yenu kama vile watu wanavyoitana watu kwenye sahani ya chakula. Akasema mwenye kusema je ni kutokana na uchache wetu zama hizo? Akasema laa bali nyinyi zama hizo mtakuwa wengi lakini mtakua kama povu la mafuriko.. hapo MwenyeziMungu ataondoa kwenye mioyo ya maadui zenu khofu juu yenu na kutia kwenye nyoyo zenu Wahn… akauliza mwenye kuuliza: ewe mtume wa MwenyeziMungu na nini wahn? Akasema ni kupenda dunia na kuchukia kifo.”

[Sunan ya Abi Daud]

Si lengine bali tu ni nuru ya uongofu inayoweza kuutakasa ulimwengu kutokana na uchafu huu na kuufanya kuwa pahali bora zaidi, nuru hii hii ambayo wapenzi wa giza(illuminati) wanaichukia, na hivyo basi kuwalazimu kutaka kuizima nuru(Uislamu) hii kwa kuimulikia giza lao kwa mbinu za kuupa Uislamu sura za ugaidi na vile vile kuupa Ugaidi sura za Uislamu-ili wapate kuupiga vita Uislamu kwa madai ya kupambana na ugaidi-vita dhidi ya ugaidi.Vita ambavyo wanapigana kwa umoja wakiwa mataifa yaliyoungana, baada ya kukusanyana.

Pia wanataja Ushindi(Nusra) lakini kwa niya tu ya kuipoteza jamii ya kiislamu. Kiujanja wanailaza jamii ya kiislamu kwa kuifikirisha kuwa Ushindi wapatikana kupitia wingi wa waislamu na wingi wa misikiti mtawalia. La sivyo, bali tu ni kwa mbinu ya kisiasa kama mbinu ile ya kisiasa ya mtume ndipo Ushindi unapopatikana na hivyo basi Daula ya kiislamu kusimamishwa.

Basi tuiamsheni jamii kwa kuvunja minyororo hii ya kiakili inayotumika na hawa ma illuminati wanaokuja kwa sura za mabwenyenye ili kuwafanya watumwa binadamu ulimwenguni. Tumuitikieni muumba wetu(Allah) katika kufaulisha matakwa yake(kuimarisha nuru yake), na kwa hakika Allah atatusaidia katika mapambano haya yetu ya kisiasa ili kufikia lengo kuu- Ushindi.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ

[Enyi Mlioamini! Mkinusuru  Dini ya MwenyeziMungu  Naye atakunusuruni na ataithubutisha miguu yenu.]

[Muhammad:07]

Kufanya kazi hii twahitaji sana kuwa wakweli(ikhlas), na twahitaji sana kutumia akili ambazo tayari tunazo-kwa hivyo cha kufanya sasa ni kupanda mbegu za fikra nzuri akilini mwetu na kunyunyuzia maji safi ya elimu sahihi kisha tupambane kiukweli kwa maneno na vitendo, kama kweli sisi ni wakweli[

إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ

Hakika MwenyeziMungu habadilishi hali za watu mpaka wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao

[Ra’ad :11]

Imeandikwa na Jamal Donde,

Mwanachama wa Hizb- Ut-Tahrir-Kenya.