ATUSIWEJE RASULI

Tumwa wetu Muhamadi, Khairu Mursalina,

Mithili yake abadi, hajazaliwapo mwana,

Ni kipendi cha Wadudi, na wote muslimina,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni

 

Msadikisha waadi, mtekeleza amana,

Si mvundaji ahadi, hana swifa ya khiyana,

Khulukaze ni jayidi, kattu dosari hazina,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

I swafi yake fuadi, na doa ‘meepukana,

Matendoye maridadi, ayaridhiyo Rabana,

Maasumu mahmudi, kherini aliyefana,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Risala ya Tauhidi, nayo alilingamana,

Kwa watu aliinadi,  vilivyo na kwa majinna,

Wapate kumuabudi, alepweke Maulana,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Hakufunda ugaidi, damu ovyo kumwagana,

Alikanya ufisadi, na kizazi kukatana,

Waambao yu gaidi, na Mola watapambana,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Alipigana Jihadi, kwa takwa la Subuhana,

Mila mbovu kusharidi, zisiwe nao ubwana,

Ili nuru ya Wahidi, izagae kila kona,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Kutusi kwa mayahudi, mitumi wake Mannana,

Ada yao  tangu jadi, na si leo wala jana,

Ni watu wenyi inadi, na kusudi na fitina,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Ni yambo lisilo budi, kulichungato mnena,

Asinene kwa kusudi, asilofaa kunena,

Maneno yana haswadi, ima moto ama janna,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Mwenye cheo Ahmadi, khatam nabiiyina,

Vivyo twamuitakidi, tulio muuminina,

Makufari mahasidi, hawachi kumtukana?

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Natufeni mashahidi, kumhami Rasulina,

Sisi kwao ndio radi, matughati wasomana,

Kuuwawa ndio haddi, kwa huyuno mtukana,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Mwenyezi ana junudi, ya siri na ya bayana,

Yenye wingi wa idadi, na sampuli ya zana,

Aliangamiza Adi, walotakabari sana,

Atusiweje Rasuli, kwa uhuru wa maoni,

 

Nitamatile muradi, hapano natulizana,

Usekula si waridi, mfumowe wa laana,

Ukilengacho zaidi, Uisilamu kuchana,

 

MTUNZI – MOHAMMED BAKARI 

ALMUFTI 

MOMBASA – KISAUNI

 

Comments are closed.