Habari na Maoni

BBI: Vipi uaminiwe na tayari hii hapa athari ya shoka lako?

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Habari na Maoni

 

Habari

Habari: Tarehe 25 Oktoba,2020 ripoti ya mradi wa ujenzi wa madaraja (BBI) ilizinduliwa rasmi katika ukumbi wa Bomas. Uzinduzi wa ripoti hii unakuja baada ya takriban mwaka mmoja tokea kuzinduliwa kwa mswada wa ripoti mwezi Novemba mwaka jana, ambapo jopo kazi lilikuwa likipokea maoni ya wakenya yaweze kujumuishwa kwenye ripoti ya mwisho. Ramani ya mchakato wa BBI ni sasa kutaundwa kamati tekelezi itakayopewa jukumu la kuihakiki ripoti hii na kuanisha vifungu gani vya kushughulikiwa kwanza kupitia ima mabadaliko ya kikatiba, bunge na sera za kiusimamizi. Mapendekezo makubwa kwenye ripoti hii haswa ni: kutanua muundo wa serikali kwa kubuni cheo cha uwaziri mkuu pamoja na manaibu wawili. Kuongeza idadi ya wabunge wa bunge la kitaifa kutoka wa 349 hadi 360. Na maseneti nao kuongezwa kutoka idadi ya sasa 67 hadi 94.

Maoni:

Ripoti ya BBI ni fikra iliozaliwa kwa zoezi muhimu la kupeana mikono’ rais Uhuru Kenyatta na aliekuwa waziri mkuu Raila Odinga. Tokea ripoti kukamilishwa na kutolewa na kamati husika kumeibuka mijadala mikali na wasiwasi mkubwa kuhusu je mapendekezo ya BBI yatafanya maisha ya raia kuwa magumu zaidi au kuyafanya mazuri. Mbali na haya, huku rais Uhuru Kenyatta,akionekanwa kwenye mikutano akiwataka wakenya kuunga mkono BBI naye makamu wake  William Ruto amekuwa akizunguuka sehemu mbalimbali nchini huku akiandamana wandani wake wa kisiasa kujifanyia kampeni ya uchaguzi wa 2022 akinadi mwito wake Huslter. Wawili hawahawa kwenye uchaguzi uliopita walikuwa wakizunguka pamoja huku wakinadi mwito wao wa ‘Tuko pamoja’ lakini baada ya miaka miwili tayari wanaonekanwa wakipingana huku kila mmoja akisema lake na kugawanya nchini kimirengo. Raila Odinga,naye hivyohivyo kwenye uchaguzi uliopita alikuwa ni hasimu mkubwa wa Uhuru Kenyatta aliefanya nchi kuwa na tafrani lakini sasa anamwita Uhuru kaka. Hii kwa hakika inaonesha wazi kwamba katika siasa ya Kidemokrasia maadui wa kudumu wala marafiki wa kudumu bali kilichoko ni maslahi tu ya kudumu.

Ama mapendekezo ya kupanua mfumo wa serikali hii inaonesha wazi jinsi tabaka la kisiasa ndio pekee ndio litakalofaidi na kunufaika na serikali kubwa na wala sio raia wa kawaida. La kupaswa kufahamu, ni kwamba wakatati kuna kuja mapendekezo,tayari wabunge wa Kenya bado wanabakia kuwa ndio wanaopekea mishahara mikubwa ulimwenguni zaidi hata kuliko wenzao wa mataifa yalioimarikia kiuchumi. Bila shaka raia  kawaida ndie atakayekamuliwa kufidia serikali hio kubwa. Huu ndio uhalisia wa siasa ya kimaslahi ya kibinafsi ya Kidemokrasia ambayo siasa kwake imekuwa ni mradi mkubwa wa biashara kwa wanasisa. Kuweko na Serikali kubwa haijalishi lolote kwani maslahi ya raia wa Kawaida ndani ya Demokrasia huwa mangati tu. Hali ya wale wanaounga mkono BBI miongoni mwao na hali ileile ya wale wanaoipinga. Tabaka zote mbili hizi ni kuchuana tu kwenye kung’ang’ania madaraka tu wala sio lengine lolote.

Ripoti ya BBI inaorodhesha matatizo mengi lakini imeshindwa kufichua kiini hasa cha matatizo yote hayo. Changamoto kubwa inayokabili nchi ni kukumbatia kwake mfumo ulio oza wa kibepari. Kwa hivyo,hakuna chochote katika yaliyopendekezwa kitakachobadilisha kimsingi hali halisi. Fauka ya haya wale waliobuni na kutengeza BBI hawatotatua matatizo ya Kenya kwani haohao ndio wenye kuleta matatizo hao ni sawasawa na ule msemo wa Kiarabu wenye maana yanayosema;vipi nitakuamini tena ilhali hii hapa athari ya shoka lako.

Taifa la Kenya na Ulimwengu kwa ujumla linahitaji mfumo uliokita barabara kiitikadi wa Kiislamu, ulio na itikadi nzito ilio na sheria zinazotoka kwa MwenyeziMungu SWT Muumba wa Mwanadamu, ulimwengu na uhai. Kwa msingi huu imara, ndio serikali yake husimamishwa pamoja na utaratibu wa kiuchumi na kijamii. Isitoshe, kupitia itikadi hii watu wote hufangamanishwa na kuwa ni umma mmoja wote wakiwa ni waja wa MwenyeziMungu (swt). Hivi ndivyo, Uislamu kwa karne kadhaa chini ya Khilafah ilizalisha wanasiasa wachamungu walio na utashi wa kisiasa uliowawezesha kulete ustawi mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.  Tuna imani kubwa kwa Inshaa Allah Khilafah itakuja hivi karibuni kuongoza ulimwengu kwa siasa za ukweli na kueneza ukweli na uadilifu kwa dunia nzima.

Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya

31/10/20