Jumla

Enyi Ndugu zetu Waislamu Wanajeshi Mukhlisina: Ramadhan Inatuwacha na Ilhali Hamujatoa Nussrah!

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Umbile la Kiyahudi ambalo limeivamia na kuikalia kimabavu ardhi yetu tukufu ya Palestina iliyo na kibla chetu cha kwanza Masjid al-Quds, mnamo Jumamosi, 4 Mei 2019 siku mbili kabla kuanza kwa Ramadhani  ya Mwaka 1440H / 2019M, liliendeleza uhayawani wake dhidi ya Ummah mtukufu wa Kiislamu kwa kuwamiminia mizinga na mabomu na kuwaua wengi ikiwemo mtoto mchanga pamoja na mamake aliyekuwa mjamzito! Nako Syria hususan mji wa Idlib, Urusi kwa ushirikiano na Iran na Jeshi la Bashar al-Assad wamezidisha mashambulizi kutoka angani na ardhini dhidi ya Waislamu wanaopigania haki yao ya kuondosha utawala wa kidhalimu wa kisekula wa kirasilmali ili watawaliwe na Uislamu chini ya serikali ya Khilafah. Ilhali ndani ya Libya na Yemen, Waislamu wanaendelea kupiganishwa kwa mujibu wa mirengo miwili; mmoja ukiongozwa na Marekani  mwengine  na Uingereza/Umoja wa Ulaya; kila mmoja akilenga kupata maslahi yake kwa kutumia mikono na damu za Waislamu!

Ndugu zetu wa Kashmir, Somalia, Afghanistan, Iraq, Crimea, Uzbekistan, Myanmar (Rohingya), Xinjiang (Uyghur) n.k wanaendelea kuishi chini ya ukandamizaji usiokuwa na mfano ukiongozwa na watawala walio na mikono ya chuma wakitawala kwa mujibu wa sheria na sera ovu zinazochorwa na kupitishwa na wakoloni Wamagharibi! Ama duniani kote viumbe vyote vinaishi kwa idhilali si wanadamu si wanyama si miti n.k vyote vimo katika kuhisi machungu yanayotokana na majanga yanayoendelea kusababishwa na mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake chafu!

Hali hii ya utumwa na ukandamizaji kattu haiwezi kuondoka mpaka pale enyi ndugu zetu Waislamu wanajeshi mukhlisina muliojaa ndani ya kambi za kijeshi katka ardhi za Waislamu mfano Pakistan, Saudi Arabia, Bangladesh, Misri, Tunisia, Sudan n.k mutakapoamua kutoa Nussrah (nguvu za kijeshi). Nussrah hii iwe haina masharti kwa anayepewa na lengo la kuitoa iwe ni kwa ajili ya kuunusuru Uislamu, Waislamu na ulimwengu kwa ujumla kwa kutawalisha Shari’ah (Qur’an na Sunnah) pekee juu ya mgongo wa ardhi. Na ilhali wanaotoa nussrah hesabu zao ziwe tu kwa kutafuta radhi za Mola (swt). Enyi Ndugu zetu Waislamu Wanajeshi mukhlisina mutaweza kuchukua hatua hiyo ikiwa watamuitikia Mwenyezi Mungu (swt) kama  alivyosema:

(يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمۡ لِمَا يُحۡيِيڪُمۡ‌ۖ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Enyi ndugu zetu Waislamu wanajeshi mukhlisina munayo mifano ya kuigwa kutoka miongoni mwa maswahaba (ra) –Ansar waliomnusuru Mtume (saw), Uislamu na Waislamu (Muhajirun) mmoja wao akiwa Sa’d ibn Mu’adh (ra) ambaye aliyefariki akiwa na umri wa miaka 37 na imepokelewa kutoka kwa Jabir (ra) kuwa alimsikia Mtume (saw) akisema: “Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu  kilitingishika kwa kufa Sa’d bin Mu’adh.” [Bukhari, 3803 na Muslim, 2466a/b] na imepokelewa kutoka kwa Ibn Umar (ra) kuwa alimsikia Mtume (saw) akisema: “Sa’d ndiye ambaye kifo chake kilitingisha Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu na milango ya mbingu kufunguliwa na malaika elfu sabini kuhudhuria mazishi yake.” [Nasai, 2055].

Daraja na utukufu waliyopewa Ansar ni kwa sababu ya kutoa nussrah na si jengine! Hivyo basi, enyi ndugu zetu Waislamu wanajeshi mukhlisina mlioko ndani ya kambi za kijeshi katika ardhi za Waislamu; tunawalinganieni mutoe nussrah kwa Hizb ut Tahrir ili kwa pamoja tusimamishe serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Itakayo kuwa mlinzi na ngao dhidi ya maadui wa Uislamu, Waislamu na wanadamu kwa jumla. Hakika kuzembea kwenu kunaendeleza ukandamizaji na umwagaji damu tukufu za wanawake, wazee na watoto wetu. Wakati umewadia wa kuwang’oa madarakani watawala vibaraka wa wakoloni ambao mnawalinda wakitekeleza uovu wa kila sampuli mbele ya masikio na macho yenu.

Tukiwa katika Mwezi huu uliojaa baraka wa Ramadhani, ndani ya kumi la pili la Maghfira (msamaha). Enyi ndugu zetu Waislamu wanajeshi mukhlisina wakati ni huu wakutaka msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ili awasamahe madhambi yenu kutokana na kuzilinda dola hizi ambazo chimbuko lake ni Makubaliano ya Sykes-Picot! Patilizeni fursa kwa hakika hakuna kheri katika kufa kifo cha kijahiliya kwa kuwalinda watawala Ruwaibidha pasina na ahadi ya utiifu kwa Khalifah anayetawala kwa Shari’ah (Qur’an na Sunnah). Kupitia nyinyi tutafaulu kwa mara nyingine tena kuwa Dola Moja, Ummah Mmoja chini ya Kiongozi Mmoja mchamungu anayetujali na kutupenda kwa kutuombea kheri nasi tukimjali na kumpenda kwa kumuombea kheri kinyume na watawala tulio nao leo! Pigeni hatua moja nasi kama Ummah wa Kiislamu tutakuwa nyuma yenu bega kwa bega kwa asilimia 100. Hakika tumechoshwa na ukandamizaji na ukazanishaji wa vitanzi shingoni mwetu! Kwa pamoja  tukizingatia maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) aliposema:

(وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)

“Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.” [Al-Anfal: 10]

 

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Makala Na.45: Ijumaa, 12 Ramadhani 1440 | 2019/05/17