Habari na Maoni

FULIZA –M-PESA RIBA INAYOFULULIZA

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Habari na Maoni

Habari: Wakenya walikopa kutoka  kwa mfumo wa FULIZA wa Safaricom  shilingi Bilioni 1.32 kila siku hii ikiwa ni kati ya mwezi April na Septemba mwaka huu jambo linaloonesha wazi hali ya wakenya kutegemea mikopo kwa matumizi yao ya nyumbani. Hili lilidokezwa na shirika la Safaricom siku ya Jumatano tarehe 10 Novemba mwaka huu ambapo faida ya shilingi bilioni 37.055 iliandikishwa na Safaricom kwa nusu ya mwaka hadi mwezi wa Septemba iliongezwa zaidi na mapato ya M-Pesa. Ripoti ya matokeo ya kifedha ya shirika la Safaricom yanaonesha kwamba katika kipindi cha siku183 pekee shirika hili liliweza kusambaza bilioni shililingi 242.6 ambayo hii ni asilimia 62.4 nyongeza ya kipindi sawa na hicho mwaka jana pale ilipotoa mkopo wa kitita cha shilingi bilioni 149.4 kupitia FULIZA.

Maoni:

Wazo la kuweka mfumo wa kuwezesha wakenya masikini na hata wenye pato la kadri, kupata mikopo kwa haraka nchini Kenya liliundiwa neno rahisi kulitamka la Kiswahili linalofahamika kama FULIZA kutoka kwa kitenzi cha kufululliza.  Kampuni ya Safaricom inayomilikiwa na Kampuni kubwa ya mawasiliano ya Uingereza Vodafone, ilizindua rasmi mpango wa Fuliza mwaka 2019 unaomilikiwa na mashirika ya kifedha matatu Safaricom yenyewe na benki ya KCB ikimiliki kiwango sawa cha asilimia 40 huku benki ya CBA ikimiliki asilimia 20. Mpango huu huruhusu wateja wa Mpesa kufanikisha miamala yao ya kifedha endapo wanakabiliwa na uhaba wa fedha kwenye akaunti zao za Mpesa.

Fuliza ni mpango wa huduma ya kifedha kwenye akaunti yako ya MPESA inayokuwezesha kununua au kumpata mkopo kupitia kwa Mpesa hata kama una uhaba wa senti. Ni mfumo maarufu wa Safaricom wa ukopeshaji unaoruhusu wateja kupata mkopo kupitia akaunti zao za Mpesa kufidia mapungufu ya fedha na mkopo huu unaofuata viwango vilivyowekwa. Kwa kiwango cha Riba inayotozwa cha asilimia 1.1 na ada ya huduma ya shilingi 30 kila siku, hudumu hii ya Safaricom imevutia wakenya zaidi ya milioni 1.4 wanaokopa kila siku. Kiwango cha mkopo kinachokadiriwa kiasi cha kitita cha shilingi Bilioni 1.34, huku Safaricom ikitaja kwamba ilipata nyongeza ya bilioni 1.2 wakopaji ambacho kwa muda wa miezi sita hadi Juni mwaka huu hii ikiashiria upungufu wa mapato kwa wakenya unaowasukuma kutegemea madeni ya gharama ya muda mfupi.

Kwa ushindani wa soko na mabadiliko ya mara kwa mara ya uchumi wa mtaji, mara kwa mara Riba hubadilisha sura yake mbaya.  Miamala ya riba ambayo ni sawa na unyonyaji mkubwa wa jasho la watu na kuhujumu biashara ni yenye kwenda kinyume na Uislamu. Sheria ya Kiislamu imeainisha kwamba aina yoyote ya mapato ya ziada kwenye huduma za mikopo ni Riba. Hali zinazobadilika za riba na bima ya mipangilio mipya ya kifedha ya Kirasilimali na taasisi zake mbovu za kifedha zenye kuwa mapato yaliyopangwa kunaendelea kuwapata Waislamu kuwa hali tata wasijue msimamo halisi wa Kiislamu juu ya miamala hii.

Fuliza inaendana kikamilifu na muamala wa Riba hivyo kulingana na Uislamu aina hii muamala haufai  kama ilivyoainishwa katika Qur’ani Tukufu na Hadith za Mtume  (ﷺ). Fuliza inaingia katika aina ya Riba iitwayo Riba Nasiia  ilioshamiri kwa zama za ujahilia ambayo mtu alitakikana kulipa malipo ziada ya ule mkopo aliupokea. Aina hii ya riba inatokana na riba iliyoamuliwa mapema ambayo mkopeshaji hupokea nyongeza ya kiasi cha alichokopesha. Ukopaji wa  Fuliza ni  aina ya riba inayotozwa mikopo ambayo leo imesheheni kote  ulimwenguni.

Riba ambalo ni tamko la kiarabu na kilugha humaanisha ziada,ongezeko au ukuaji. Kiupande wa kisheria  Riba humaanisha kiasi cha ziada cha pesa apatacho anayekopesha. Aidha ziada yoyote aitoayo mkopaji kwa mkopeshaji. Kwa uchumi wa leo, riba huzunguka kama bei ya mkopo uliokopeshwa ili mtu aweze kupata mkopo huo. Katika mfumo wa benki leo kuingia kwa riba ya kinyonyaji kumegeuza pesa kuwa bidhaa ya biashara.

.

Al Imam Ghazal alisema: “Kufanya biashara ya pesa kwa lengo la kupata riba kunafanya pesa iwe ni bidhaa ya sokoni.Kushiriki aina hii ya biashara ni moja ya njia za unyanyasaji’ na sisi twajua wazi adhabu kali kwa wanaoamiliana na miamala ya riba. Kula riba ni moja wapo ya madhambi saba makuu yenye kuangamiza na ni sambamba na Shirk, uchawi, kuuwa nafsi iso na hatia, kula mali ya mayatima, Kukimbia kwa uwanja wa mapambano (vita) na kumtuhumu kwa zinaa mwanamke mwenye staha.

Hakika ya wanaofanya miamala ya riba huibia watu mali zao kama vile ni miongoni mwa njia mbovu  na biashara mbaya wanasubiriwa na adhabu ya moto.

ٱلَّذِينَ يَأْكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِى يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيْطَٰنُ مِنَ ٱلْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلْبَيْعُ مِثْلُ ٱلرِّبَوٰاْ ۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلْبَيْعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْ ۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ

 Wale wanaokula riba, hawasimami (kuendesha yao) ila kama anavyosimama yule ambaye Shetani kamzuga kwa kumsawaa; (wako mbioni tu, hawana kituo). (Na) haya ni kwa sababu wamesema, “Biashara ni kama riba”, bali Mwenyezi Mungu · ameihalalisha biashara na kaiharimisha riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake (ya huku kukatazwa riba), kisha akajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) yaliyopita (aliyokwisha yapata); na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.

TMQ 2.275

Ni muhimu kutambua kwamba Ummah unakabiliwa na matatizo ya kiuchumi na  mashambulizi mengi ya fikra kutoka kwa hadhara ya Kimagharibi. Hili limeufanya ummah kukumbwa na matatizo ya kiuchumi ya mfumo wa Kirasilimali ambao uchumi wake umekita kwenye mizizi ya riba .  Hivyo   kazi kuu leo ni kuhuisha Ummah, kwa ipa fikra sahihi za Kiislamu.

Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir Na

Shabani Mwalimu.

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya