Jumla

Hajj Na Jihad ni Mapacha Wawili

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Anaelezea Mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Bin Khalil Abu Rashtah katika tafsiri yake ya surat al-Baqarah aya ya 189-190 kwamba yanabainika mambo yafuatayo:

Baada ya Allah kutaja mambo ya Hijja katika aya 189 kisha akataja mambo ya Jihad katika aya 190 kisha akarudia tena kuitaja Hijja. Allah Mtukufu Ameambatanisha utajo wa Hijja na Jihad katika aya nyingi ndani ya Quran.

Baada ya kutaja Jihad katika 184 akafuatisha Hijjah na Umra katika aya 158 Surat al-Baqara. Na baada ya kutaja habari za Hijja kuanzia aya 26 surat al-Hajj baada ya hapo akataja aya za Qitaal kuanzia 38 hadi 41 kanakwamba shida na uzito unaopatikana katika safari ya Hijja na pamoja na uzito ulioko katika Jihad inabainisha hikma ya kutajwa Jihad na Hijja kwa pamoja.

Na kanakwamba msamaha wa Hijja iliyotakabaliwa na shahada katika njia ya Allah inabainisha mahusiano makubwa yaliyopo baina ya Hijjah na Jihad.

Kisha mama Aisha (ra) alipomuuliza Mtume (saw) kuhusu kutofaradhishwa Jihad kwa wanawake, Mtume (saw) akasema:

عليكنن جهاد لا قتال فيه الحج والعمرة

Hakika ni juu yenu Jihad isiyo na vita: nayo ni Hajj na Umra.

Na Mtume (saw) alipohiji mwaka wa kumi baada ya Hijra (Hijja ya kuaga) baada ya Mtume (saw) kukamilisha na kuwabainishia Waislamu ibada za Hijja katika mambo ya mwanzo aliyoyafanya Madina ni kuandaa jeshi la usama kuwapiga vita Warumi yaani Jihad ndio ilikuwa miongoni mwa kazi zake aliporudi Madina kutoka Hijja.

Na kadhalika Sayyidna Abubakar (ra) alihiji mwaka wa 12, na alipokamilisha Hijja yake na kurudi Madina miongoni mwa kazi zake za mwanzo ni kupeleka majeshi kuwapiga vita Wafursi na Warumi kisha vikaja vita vya Yarmuk ambavyo alikufa Abubarak (ra) vita vikiwa vinaendelea.

Kisha akahiji Khalid (ra) vita vya Iraq vikiwa vinaendelea, na alipokamilisha ibada yake akarudi na kuikamilisha Jihad yake.

Na Sayyidna Umar (ra) alihiji mwaka wa 14 na ndani ya Hijja yake aliwatoa Waislamu kuwapiga vita Wafursi.

Na hivyo ndivyo walivyokuwa wakifanya baadhi ya Makhalifa waongofu, ikawa baadhi yao wanapigana mwaka na wanahiji mwaka kanakwamba kati ya Jihad na Hijja kuna mahusiano na makubaliano.

Hii ndiyo Hijja na Jihad katika kitabu cha Allah na katika Sunnah ya Mtume (saw) na katika Seerah ya Makhalifa waongofu na waliowafuata katika Makhalifa wema, ilikuwa misafara yao ya kwenda Hijja inaambatana na misafara ya majeshi kwenda kuwapiga vita maadui zao.

  فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيّاً

Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio; Basi watakuja kuta malipo ya ubaya. [Maryam: 59]

Wakatenganisha kati ya hukmu za Kiislamu, wakaruhusu kiwango fulani, kuwalingania katika ibada ila wakanyamaza kimya kuhusu ulinganizi wa Khilafah na Jihad, wakatenganisha kati ya Sala na Khilafah, na suala la kwenda Hajj pamoja na misafara ya majeshi ya kwenda Jihad, bali wamefikia kiwango cha kuisitisha Jihad, na kudai Jihad ya amani,

قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa?