Taarifa za Eneo

Hizb ut-Tahrir/Kenya yazindua rasmi kampeni chini ya kauli mbiu: Kila mmoja wetu ni mchungaji.

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Janga la virusi vya Corona linaloendelea kuuwa watu wengi duniani  limepelekea pia usitishwaji wa harakati nyingi za kiuchumi hivyo kusambaratisha hali ya maisha ya watu. Janga hili aidha, limefanya shule na taasisi nyingi za elimu kufungwa, hatua ambayo pia imezalisha janga jengine nchini Kenya; ongozeko kubwa la mimba kwa wasichana wa shule. Kwenye utafiti wa hivi karibuni juu ya mimba za wasichana, umeonesha kuwa zaidi ya banati 152,820 wametungwa mimba kote nchini tokea shule kufungwa. Takwimu hizi japo kwamba Serikali imezitaja kuwa zimetiwa chumvi lakini ukweli wa mambo ni kuwa uovu huu matendo ya ngono ni wenye kushamiri katika jamii ya Kisecular

Kwa kulichukulia unyeti wa suala hili, Hizb ut-Tahrir Kenya inaanzisha kampeni kubwa nchini ya kauli mbiu: “Kila mmoja wetu ni mchungaji” itakayoanza tarehe 25 Agosti 2020 na kuendelea hadi 31 Desemba,2020.

Msururu wa amali kwenye kampeni hii unajumuisha, mihadhara misikitini, matembezi ya mitaani, mijadala hai miongoni mwa amali nyengine. Mada kubwa katika mazungumzo ikiwa ni jinsi gani mfumo wa kirasilimali na itikadi yake mbovu ya Kisecular ilivyochangia sio tu janga hili la kijamii bali majanga yote katika nyanja zote za maisha. Umma ambao pia hujumuisha wazazi na wasimamizi wa watoto utakumbushwa majukumu walionayo ya kulinda watoto wao kutokana na uvamizi wa tamaduni za kimagharibi kwa kuhakikisha kuwa wanaunda utambulisho halisi wa Kiislamu kwa watoto.

Tunaomba jamii kuungana nasi katika kampeni tukizingatia kuwa ni sehemu ya kazi tukufu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Fuatlia Kampeni kwa Hash tagi: Follow the campaign hashtags:

#Covid-19 _Inafichua Urasilimali

 #Covid -19 _Usekula _ unatenganisha Dini  

 #Covid-19   Majanga ya umma _Hupatilizwa Na warasilimali kupata faida.

 Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa vyombo vya Habari

 Hizb ut Tahrir in Kenya