Ujumbe wa Ameer

Khutba ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Munasaba wa matukio mawili. Kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1438 Hijiria/ 2017 Miladia. Na Uzinduzi wa Chaneli ya TV ya Al-Waqiyah.

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Sifa njema ni zake Allah (swt) na Sala na salamu zimfikie Mtume (saw), Familia yake, masahaba zake na wote wanaomfuata…

Wapendwa Waislamu, ndugu zangu wapenzi wabebaji daawa, wapenzi watazamaji na wapenzi wasikilizaji na kwa wote wenye nyoyo za unyenyekevu na wanaosikiliza kwa makini,

 Asalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Ndugu zangu wapenzi mabwana na mabibi, nakupeni habari njema katika usiku huu wenye baraka kwa kuadhimisha matukio mawili muhimu sana:

Kwanza: tukio la kujiliwa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani:

Baada ya kufuatilia kwa makini suala la mwezi mtukufu wa Ramadhan usiku wa leo Jumamosi tarehe 27/5/2017 muandamo wake umethibitishwa na kukidhi vigezo vya kisheria katika baadhi ya Nchi za Waislamu, hivyo basi kesho Jumamosi ni siku ya mwanzo ya kuanzia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kutoka kwa Bukhari kutoka kwa Muhammad bin Ziyad alisema”nilimsikia Abu Huraira (ra) akisema Mtume(saw) sala na salamu ziwe juu yake na familia yake, alisema: Abu Al Qassim (saw):

«صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فأَكْمِلُوا عِدَّةَ شعبانَ ثلاثين»

“Fungeni kwa kuonekanwa kwa mwezi na fungueni kwa kuonekanwa kwa mwezi, na kama kutakuwepo na mawingu (yakakuzuwiyeni musiuone mwezi ) kamilisheni siku 30 za Sha’ban”

 

Allah (swt) kaufanya Mwezi huu Mtukufu ni mwezi wake na anawalipa wanaofunga thawabu anazozitaka, yaani thawabu zisizokuwa na idadi.  Katika hadith Qudsi Mtume (saw) Anasema:

«كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ لَهُ إِلَّا الصَّوْمَ، فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ»

“Amali zote za wanadamu ni zao wao isipokuwa funga ambayo ni yangu mimi, na mimi ndiye nitakayewalipa”.

Huu ni mwezi makhsusi katika tareekh ya Kiislamu, ambao ndani yake iliteremeshwa Quran Tukufu:

 [شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ]

“Ni ndani ya mwezi wa Ramadhan ndio ambao imeteremshwa Quran, ili iwe muongozo kwa watu na hoja zilizowazi na upambanuzi” (wa baina ya haki na batil) (Al Baqara: 185)

Katika mwezi huu Waislamu walishindana katika kutenda mema kwa sababu matendo mema katika mwezi huu yana thawabu na ujira mkubwa zaidi, na huku wakitafuta msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa kufunga kwa ikhlasi na kujitolea kidhati.

Katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abu Huraira (ra) kutoka kwa Mtume (saw) amesema:

«مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ، وَمَنْ قَامَ لَيْلَةَ القَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»

“Yoyote atakayefunga mwezi wa Ramadhan kwa imani thabiti na kutarajia malipo yake kwa Mwenyezi  Mungu basi atasamehewa madhambi yake yaliyopita, na yoyote atakayehuisha ibada katika usiku wenye cheo, akiwa na imani thabiti na akitarajia malipo kutoka kwa Allah basi atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.”

Makhalifa na Mawali katika Dola ya Kiislamu walikuwa wakihifadhi usalama wa nchi na watu wake, na waliusambaza Uislamu duniani kote kwa njia ya Da’wah na Jihad. Makhalifa waliwaongoza Waislamu kwa sheria za Allah na waliwaongoza katika Jihad kwa ajili ya Allah, jeshi lao lilisafiri kupitia majangwa makubwa na joto kali, na merikebu zao zikapambana na mikondo ya mawimbi makali katika njia ya kulifanya neno la Allah liwe juu na kueneza haki na uadilifu ulimwenguni kote. Majeshi yao yakiikhutubia bahari kwa kuieleza: “Lau tungejua kama kuna ardhi yenye kukaliwa na watu nyuma yako, basi tungevuka bahari kwenda kusimamisha bendera ya Uislamu”. Aidha, Makhalifa nao walikuwa wakinadi wakiyambia mawingu ya mvua: “Ewe mvua! nyesha popote utakapo, kwa kuwa popote utakaponyesheza utakayoimwagilia ni ardhi ya Waislamu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu” Waislamu walisimama nyuma ya kiongozi wao Khalifa wakimuunga mkono afanyapo mema/mazuri na wakimuhisabu anapokosea, kwani walifahamu kuwa wao na Khalifa ni sawa mbele ya sheria.

Umma, serekali na jamii wote walikuwa wakiharakishwa kwa Uislamu na kuunganishwa nao. Waliikaribisha Ramadhani kwa furaha isiyo na kifani na moyo mkunjufu, na waliiaga kwa majonzi na masikitiko, na wakiomba wakutane nayo tena kwa mara nyengine, ili wapate matukufu yaliyomo ndani ya Ramadhan, kwa kupata mafanikio ya duniani na akhera, na huko ndiko kufaulu kukubwa. Tunamuomba Allah (swt) Aufanye mwezi huu uwe wa kheri kubwa na baraka tele kwa Waislamu wote, na ikifika Ramadhan ijayo tuwe tayari tunaishi ndani ya Dola ya Kiislamu ya Khilafa Rashida. Ni Khalifah ndie atakaeshughulikia suala la kuandama kwa mwezi, na ndie atakaewatangazia Waislamu kuanza kwa Ramadhan, na kuirejeshea tena Ramadhan hadhi ya kuwa mwezi wa ushindi na Jihad pamoja na barka na rehma kwa Waumini.

Wakati huo Ramadhan itakuwa tena chini ya kivuli cha Khilafah, na nuru yake itarejea na kung’ara tena. Na itarejea tena kuwa mwezi wa ibada na Jihad. Na Takbir zake zote mbili zitarejeshwa ; Takbir ya Muadhini ya kutujuza muda wa kufuturu (Iftar), na Takbir za Mujahidina ikitujuulisha ushindi. Na hilo lipo karibu kwa idhini na tawfiki ya Allah Inshallah.

  إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا

“Kwa yakini Allah Anatimiza kusudio lake (lolote alitakalo hakuna wa kumpinga) hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo chake (At-Talaq: 3)

Habari njema ya pili ambayo ningependa kuwafikishia ni uzinduzi wa Chaneli ya Runinga ya Al-Waqiyah ndani ya usiku huu mtukufu. Leo hii mti wa Habari  wa Hizb ut Tahrir umetoa matunda yake. Umezaa matunda yenye siha na rutba yanayofurahisha macho na yanayotuliza nyoyo. Ni tunda na tija itakayolinda hadhira yake dhidi ya ghilba, uongo na upotoshaji. Itaitangaza haqi na kuifedhehi batil. Ni tunda litakaloshuhudiwa na macho na kung’arisha fikra, ni tunda litakalozaa kheri kwa hadhira yake na wote wenye nyoyo na usikivu makini. Ni tunda linaloitwa Waqiya (Mlinzi) na ni mlinzi kwa maana yake, jina zuri lilioje pamoja na maana yake. Kwa kuwa itaonesha njia na kuonesha usahihi wake kwa kushikamana na haqi na kuitangaza. Ni tunda litakaloleta kheri kwa watu wake na kwa watu wengine watakaosikiliza kwa mazingatio.

 [قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

“Sema hii ndio njia yangu ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ujuzi wa kweli, nafanya (kazi hii) mimi na wanaonifuata”. Na utakatifu ni wa Allah, nami sio miongoni mwa washirikina” (Yusuf: 108)

Kwa kukhitimisha, nazindua kwa jina la Allah faraja yetu hii (Al Waqiyah) ili iweze kuunganisha viungo viwili navyo ni matangazo na gazeti la Ar-Raya, ambayo vitafanya kazi bega kwa bega katika kupaza kwa nguvu taarifa za ukweli kupitia audio na video, na kupitia machapisho na video ili kusafisha uoni, kuhuisha nyoyo na kueneza kheri duniani kote pomoja na kuinua Uislamu daraja ya juu ya mifumo yote.

[أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ]

“Jee hukuona jinsi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri ambao mizizi yake ni imara na matawi yake yametandawaa mawinguni”(Ibrahim: 24)

Na mwisho wa kauli yetu tunasema: Shukran zote anastahiki Mwenyezi Mungu. Mola wa walimwengu wote.

 

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Amiri wa Hizb ut-Tahrir

 

Jumamosi, 1 Ramadhan 1438 Hijiria/ 27 05 2017 Miladia