Habari na Maoni

Kifo cha Mugabe: Sio Mwisho wa Mkono wa Ukoloni

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Habari:

Viongozi wa dunia waliomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwa Robert Gabriel Mugabe aliyefariki huko Singapore mnamo 6 Septemba 2019 akiwa na umri wa miaka 95. Mrithi wa Mugabe, Rais Emmerson Mnangagwa alitangaza kifo cha Mugabe, alimsifu kama “mwakilishi wa ukombozi.” Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa zamani Mwai Kibaki wote walimtaja kama “kiongozi mwenye ruwaza aliyepigania ukombozi Waafrika. Msemaji wa Boris Johnson alisema: ‘Sisi kwa hakika tunaelekeza rambirambi zetu kwa wanaomboleza lakini twajua kwamba kwa wengi alikuwa ni kikwazo cha ufanisi wa siku zijazo…’

Maoni:

Dunia imegawanyika katikati kuhusu kumbukumbu za kiongozi ambaye alijulikana kama shujaa katika enzi za ukoloni ambaye alibadilika na kuwa dikteta mwagaji damu ambaye utawala wake wa miaka 37 uliisha kwa mapinduzi mnamo 2017. Aliwekwa jela na kuteswa chini ya utawala wa weupe-wachache wa Ian Smith wakati wa Rhodesia. Mugabe alionekana na Waafrika wengi kama mkombozi mtajika na mabwana zake wakoloni Waingereza waliwahi kumpa cheo kama mwanamapinduzi. Katika makubaliano ya Lancaster House mnamo 1979 huko London yalipelekea uhuru wa Zimbabwe na Mugabe akirudi nyumbani kama shujaa.

Maisha ya Robert Mugabe yamefichua fahamu za kirongo za uhuru. ‘Upiganiaji wa uhuru’ kutoka kwa Waafrika ‘mashujaa’ ambao walibandikizwa kuwa wakombozi ambao baadaye walikuja kujulikana kama wakandamizaji. Tangu kuingia mamlakani, harakati za kupambana na ukoloni ndani ya nchi za Afrika kama Zimbabwe, Angola, Mozambique, Namibia na Afrika Kusini zimebakia katik udhibiti wa jamii za walowezi wakoloni. Wazungu mabwana wakoloni walifanya kazi kikamilifu kubadilisha utawala wa nguvu wa watu weupe na kuweka utawala wa wenyeji weusi ili kuendeleza ukoloni. Harakati za Afrika ziliungwa mkono na kuongozwa na mabwana wale wale wakoloni. Chini ya bendera ya kujitawala, Bara la Afrika likaletewa nidhamu mbadala ya kujitawala na fikra za demokrasia ya vyama vingi, ambazo zilibuniwa na Wamagharibi wakoloni. Lakini fikra hizi mpya zikaipelekea Afrika kuganda na kukosa amani kiuchumi, kisiasa na kijamii. Lakushangaza ni kwamba Wamagharibi wanawalaumu watawala wazee wa Afrika kwa “Maradhi ya Ukubwa” yaliyo sababisha majanga ndani ya Afrika ambayo kihakika ni natija ya nidhamu ya kiutawala ya kidemokrasia ambayo ndiyo mbovu. Hivyo basi, wakabadilisha wimbo na kuleta –ndoto mpya ya Afrika inayojulikana kama Ukombozi wa Afrika inayoelezewa kuwa kinyume cha utawala wa wazee ili kuwadanganya wajinga kuamini kwamba Afrika ina ruwaza.

Punde tu baada ya Mugabe kuingia mamlakani alikazanisha utawala ili kubakia uongozini na kuanza kuwakandamiza wanasiasa waliompinga kama Joshua Nkomo; mpiganaji wa uhuru mwenza ambaye baadaye walizozana. Kuzozana kwao kukapelekea vita ambavyo Mugabe alituma jeshi lake la Kikosi cha Tano lililopata mafunzo huko Korea Kaskazini ili kusambaratisha wapiganaji waasi waliobeba silaha waliokuwa watiifu kwa Nkomo katika mkoa wa Matebeleland ambapo watu takribani 200,000 waliuliwa.  Hivyo basi vurugu la serikali likachipuza kama njia ya kulinda uongozi kwa waliourithi dhidi ya viongozi wapinzani. Tume ya Afrika Kusini ambayo ni taasisi ya serikali ambayo ilizungumzia kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na ANC. Rais Nelson Mandela hakuona haya kuomba umma msamaha kwa waathiriwa wa ANC kufeli kuheshimu haki za binadamu. Mnamo 2008, Serikali ya Kenya iliunda tume inayojulikana kama Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano (TJRC) ili kutathmini dhulma za kihistoria na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa tawala huru.

Hakuna shaka bwana mkoloni wa Zimbawe UK ndiye aliyeweka mchakato wa kuondolewa Mugabe kwa njia ya kijeshi mnamo 2017 na kumuweka Rais Emmerson Mnangagwa kupitia bodi za eneo (SADC) na Muungano wa Afrika (AU). UK bado inadhibiti mustakbal wa Zimbabwe kupitia demokrasia ambayo imedhibitisha kufeli kiukamilifu. Watu wa Zimbabwe na Afrika kwa ujumla lazima wafahamu kwamba kifo cha kiongozi wao yeyote haimaanishi kuwa ndio mwisho wa mkono wa mkoloni. Lakuzingatiwa ni kuwa uongozi wa Afrika bado umefungamanishwa na Wamagharibi. Afrika itakombolewa kiukweli kutoka katika makucha ya ukoloni mamboleo na kiongozi mwenye ruwaza anayekwenda mbio kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kupitia utekelezaji wa Uislamu katika nyanja zote za maisha chini ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb utTahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir