Da'wah Kiulimwengu -Jumla

Maelfu ya waislamu wanaoiunga mkono Hizb ut Tahrir waandamana na kupinga muamala wa Trump na kusisitiza kua Kadhia ya Palestina ni Kadhia ya Kiislamu na ni wajib kuikomboa.

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Hizb ut-Tahrir katika ardhi tukufu ya Palestina imeandaa mkusanyiko mkubwa katika mji wa Khalil alasiri ya leo jumanne 11/2/2020 kwa ajili ya kupinga muamala wa Trump na kusisitiza kua kadhia ya Palestina ni kadhia ya kiislamu na ni wajib kuikomboa yote.

Waliohudhuria katika mkusanyiko huo walinyanyua bendera nyeupe (Liwaa) na bendera nyeusi (Raya) na mabango yalio na miito inayolingania kuharakisha majeshi ya waislamu, na wakanyanyua sauti zao dhidi ya Trump na dola za Kiarabu, pia walinyanyua sauti zao kuunga mkono kurudi kwa Khilafah ambayo itaikomboa Palestina na kuling’oa umbile la Kiyahudi kutoka mashina yake.

Daktari Ibrahim Al-Tamimi, mwanachama katika Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir Palestina alitoa kalima katika mkusanyiko huo akisisitiza kua kilichompa ushujaa Trump juu ya uovu wake ni udhalili wa dola zilizopo na njama zao dhidi ya umma……na lau Trump angelijua kwamba baina ya watawala wa waislamu leo kuna wanaume kama Harun Rashid na Swalahudin Ayub, basi asingejaribu kuingilia kadhia yoyote miongoni mwa kadhia za waislamu.

Bwana Al-Tamimi alionyesha kua Amerika ndio mama wa maovu na ndie baba wa maovu……na sio kwa waislamu pekee bali kwa wanadamu wote.. na ardhi ya Palestina sio milki ya Trump mpaka awe anampa amtakaye na kumzuia amtakaye, na sio milki ya watawala wala wale wanaopumua na kutoa ulimi nyuma ya suluhisho za kujisalimisha kwa dola za Kimagharibi….bali ni milki ya ummati Muhammad S.a.w .

Kwa kumalizia kalima yake, Daktari aliwahamasisha majeshi ya umma wa kiisilamu na kuwalingania kusimama na wajib wao kwa ardhi ya Israi ya Mtume wao S.a.w, ili waweze kuikomboa Palestina na kuzuia upuuzi wa Amerika na muamala wao na kuzikalia kwake kimabavu biladi za waislamu….. Jibu la kihakika kwa muamala wa Trump ni kuikomboa Palestina.