Jumla

Majadiliano ya Kimikakati Kati ya Nchi Mbili (BSD): Ni Njama ya Kikoloni Kuipora Kenya na Kuwapiga Vita Kimfumo Waislamu na Uislamu

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Ujumbe wa Kenya ukiongozwa na Waziri wa Masuala ya Kigeni Monica Juma na Waziri wa Ndani Fred Matiangi ulishiriki katika mkutano wa ngazi ya juu na wenzao wa Amerika ambao ujumbe wao uliongozwa na Naibu Katibu wa Wizara ya Kigeni wa Amerika, John Sullivan na Msaidizi wa Katibu wa Wizara ya Kigeni wa Amerika ndani ya Afrika, Tibor Nagy. Huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa mwaka uliofanyika kuanzia 7 – 8 Mei 2019 ndani ya Washington DC, baada ya ziara ya kihistoria ya Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumatatu, 27 Agosti 2018 kuzuru White House kwa mualiko wa Rais Donald Trump. BSD imesimama juu ya nguzo nne: kwanza-ustawi wa kiuchumi, biashara na uwekezaji, pili-ushirikiano wa kiusalama, tatu-demokrasia, utawala na usalama wa raia na nne-masuala ya kimataifa na kimaeneo. Nguzo nne hizo zinafichua asili ya udanganyifu uliopo katika kile kinachoitwa BSD yanayotokamana na mpango muovu wa Marekani ndani ya Afrika. Ili kuelewa uhalisia tungependa kubainisha yafuatayo:

Kwanza, mwito wa ustawi wa kiuchumi, biashara na kiuwekezaji si chochote tunapozingatia hali halisi inayoikumba Kenya kutokana na machungu yaliyo sababishwa na mapendekezo ya kidhalimu yanayotoka kwa taasisi za kifedha za Marekani ambazo zimeiteka nchi kuwa mateka kutokana na mikopo yake ya riba isiyoingia akilini ili kufadhili ujenzi wa miundo mbinu miongoni mwa mipango mengine!

Pili, ushirikiano wa kiusalama ina maanisha kuendeleza vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kisingizio cha kupigana na ugaidi na misimamo mikali. Tukizingatia kuwa hivi sasa Kenya imo katika vita vya kiwakala vinavyopigiwa debe na mataifa ya Kimagharibi yakiongozwa na Marekani ndani ya Somalia katika kile kinachoitwa vita dhidi ya Al Shabaab. Vita ambavyo Marekani yenyewe imefeli kabisa kuvishinda na hivyo sasa imehusisha tawala vibaraka kama Kenya, Uganda na Ethiopia miongoni mwa mataifa mengine kubuni Kikosi cha Umoja wa Afrika ndani ya Somalia (AMISOM) mnamo Februari 2007 na kushirikiana na Kikosi cha Marekani ndani ya Afrika (USAFRICOM) mnamo Oktoba 2007 ili kupigana vita vya Marekani ndani ya Bara la Afrika.

Tatu, demokrasia, utawala na usalama wa raia ina maanisha kumakinisha sera potofu zinazowapa mamlaka wanadamu kujitungia sheria kwa matamanio yao na kusimamia mambo ya watu kwa mujibu wa sheria za mwanadamu kinyume na Shari’ah (Qur’an na Sunnah) ya Muumba. Sheria ambazo zinajumuisha kupigia debe masuala ya usagaji, ushoga au (LGBT), jamii ya kisekula ya uhuru (liberali), uchumi uliosimama juu ya riba na ushuru miongoni mwa machafu mengine. Haya yataendeleza kusababisha wasiwasi na ufisadi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu.

Nne, masuala ya kimataifa na kimaeneo ni kuendeleza sera za Marekani kimataifa na kimaeneo na kuhakikisha kuwa Marekani inaibuka mshindi dhidi ya mabwana wakoloni wengine ambao pia nao wanapigiana njama dhidi yao ili kupora rasilimali za kimataifa na za kieneo.

Kwa kuhitimisha ni wazi kuwa hii BSD si chochote isipokuwa ni njama nyingine ya kuipora Kenya rasilimali zake adhimu na kuwafukarisha na kuwatia katika utumwa watu wake kutokana na sera za Marekani zilizo jificha kwa sura ya mipango ya uwekezaji. Licha ya hayo, Uislamu na Waislamu wataendelea kuhisi maumivu kutokana na ushirikiano katika miradi ya kiusalama inayobuniwa na serikali ovu ya Marekani ambayo inaliunga mkono umbile ovu la Kiyahudi ambalo limeivamia na linaendelea kukejeli matukufu yetu na kuikalia kimabavu ardhi yetu Tukufu ya Palestina ambayo ina kipenzi chetu Msikiti al-Aqsa kibla chetu cha kwanza. Kenya na Afrika ili kupata ustawi wa kweli ni mpaka wa kumbatie ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni kupitia Khilafah ndiyo Kenya na Afrika itakombolewa kutoka katika njama za mataifa ya kikoloni ya Kimagharibi kama Marekani na washirika wake ambao ndiyo chanzo cha Kenya na Afrika kuganda kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu. Khilafah itakayo ongozwa na kiongozi muadilifu Khalifah anayejituma kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) kwa manufaa ya raia wake tu.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya