Habari na Maoni

Miaka 25 ya Kumbukumbu Chungu: Msukumo wa Kutochoka katika Ulinganizi wa Kurudisha tena Khilafah Ngao na Mlinzi wetu wa Ukweli na SIO Umoja wa Mataifa

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Katika kutoa heshima kwa maelfu ya Waislamu hususan wanaume na vijana waliouliwa katika mauaji ya Julai 1995 wakati wa vita vya Balkan, António Guterres aliahidi kuwa hawatosahauliwa kattu. Alisema, “Robo karne iliyopita, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa waliwafelisha watu wa Srebrenica. Kama Katibu Mkuu wa zamani Kofi Annan alisema, kufeli huku “kutatia wasiwasi historia yetu daima.” Kwa kuongezea, alisema, “Kukabiliana na yaliyopita ni hatua muhimu katika kuelekea kujenga imani.” (news.un.org/en, 9 Julai 2020)

Maoni:

Kwa mara nyingine mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anashiriki zoezi la mahusiano na umma kwa kutoa huduma za kimazungumzo kwa uhalifu mkubwa kuwahi kutekelezwa dhidi ya Ummah wa Waislamu nyuma ya migongo ya wanaoitwa wanajeshi wa kuweka amani wa UN. Hakika, kitendo chake hiki ni kufuata nyayo za watangulizi wake ambao wameboresha sanaa ya kuigiza kama mabalozi wa amani duniani. Kiukweli ni kuwa wao ni sehemu ya mpangilio wa kisekula wa kirasilimali duniani ambao wameamua kuhakikisha damu ya Waislamu inamwagwa, heshima na hadhi zao zinapuuzwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, Uislamu wenye siasa kali na Waislamu wenye misimamo mikali! UN inabakia kuwa ni zana ya kikoloni ikihudumikia mpangilio wa kisekula wa kirasilimali!

Haijatutoka akilini mwetu kuwa chini ya uongozi wa mkuu wa sasa wa UN kwamba ndio njama na mateso kwa Waislamu yamefikia kilele kutoka kila kona ya dunia. Kwa mfano, utawala wa Uchina unaangamiza mamilioni ya ndugu zetu Waislamu Wauyghur kwa kuwatia ndani ya kambi za kinyama na kuwapa mafunzo kwa thaqafa ovu ya kikomunisti kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, misimamo mikali na kujitenga. Chuki ya utawala wa India dhidi ya Waislamu ikawapelekea kufutilia mbali Kipengee 370 mnamo 5 Agosti 2019 na kusababisha mateso zaidi kwa Waislamu wa Kashmir! Kwa kuongezea, ikapitisha Sheria ya (Mabadiliko) ya Uraia mnamo 11 Disemba 2019 ili kuwaharamisha, kuwatenga na kuwaadhibu Waislamu wanaoishi ndani ya India kwa ujumla! Mizozo, vita na mauaji kwa ushawishi wa wakoloni Wamagharibi inaangamiza nchi za Waislamu kuanzia Yemen, Libya, Somalia, Afghanistan, Eneo la Sahel, Syria, Palestina, Myanmar (Waislamu Warohingya) nk inaendelea mpaka sasa huku Umoja wa Mataifa ukitizama!

Matumaini na imani yetu ipo katika kurudisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Ni kupitia Khilafah pekee ndipo sisi Waislamu tutakapohisi amani, utulivu na ustawi wa kweli. Kwani hadhi na heshima zetu zitalindwa na kiongozi wa kweli Khalifah ambaye atakuwa mlinzi na ngao yetu dhidi ya njama zinazopigwa na wafuasi wa Shaitan wakiongozwa na Amerika leo na washirika wake ambao wanapigia debe mfumo wao batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake chafu zilizo na sumu za demokrasia, ukoloni, maadili huria, nidhamu ya uchumi kwa msingi wa riba na ushuru pamoja na maovu mengine. Hakika, «إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi (Khalifah) ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda” Msukumo wetu usiku na mchana ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutimiza bishara ya Mtume (saw): ثم تكون ملكاً جبريا، فتكون ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج النبوة، ثم سكت “…Kisha kutakuwepo na utawala wa ukandamizaji, utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu atataka uwepo kisha Mwenyezi Mungu atauondoa wakati anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume,” Kisha akanyamaza. [Ahmad]  

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir