Jumla

Misikiti Itafunguliwa Pasi na Masharti na Kulindwa na Khilafah na SIO Tawala za Kisekula

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Waislamu nchini Kenya na baadhi ya nchi duniani wamo katika tabu kutokana na misikiti yao kufungwa na tawala za kisekula kwa kisingizio cha kuwalinda Waislamu kutokamana na kuenea kwa janga la COVID-19 ndani ya sehemu za ibada. Kitendawili kilichopo nchini Kenya ni kwamba misikiti ilifungwa wakati ambapo idadi ya maambukizi ilikuwa takribani 100. Lakushangaza ni kuwa baada ya takribani miezi minne idadi imefikia zaidi ya 10,000+ na makadirio ya maambukizi kwa siku ya kiwa 200+ kwa maana yanaongezeka kila kukicha. Serikali ya Kenya mnamo 6 Julai, 2020 iliagiza lile linaloitwa Baraza la Dini Mseto linaloongozwa na Archbishop Anthony Muheria kutoa mwelekeo kuhusiana na hatua zitakazochukuliwa kwa maandalizi ya kufungua sehemu za ibada zinazojumuisha misikiti!

Hali hii imezifichua tawala za kisekula ambazo daima zinapiga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu duniani kote. Haingii akilini kusikiza hoja na sababu zinazotolewa ili kuunga mkono kufungwa kwa misikiti ilhali kila mmoja anajua kuwa misikiti ndio vituo visafi na vyanzo vya kutafuta uokozi kunapotokea majanga katika jamii. Kufungwa kwa misikiti kumewafanya Waislamu duniani kuonja yale wanayohisi na kupitia ndugu zetu Waislamu kila umbile la Kiyahudi linapoweka vizuizi na kuvamia maeneo ya Qibla chetu kipenzi, Msikiti Al-Aqsa ili Waislamu wasiweze kuswali ndani yake pamoja na mashambulizi yake mapya ambapo mahakama ya Isreali imetoa uamuzi unaoagiza kufungwa kwa lango la Bab al-Rahma la Msikiti Al-Aqsa ndani ya Jerusalem Mashariki! (menafn.com, 14 Julai 2020).  Kufungwa na kuharibiwa kwa zaidi ya misikiti 200 ndani ya Xinjiang na miji yake kujengwa upya ili kuwa sehemu za ujasusi kwa utawala wa Uchina. (bitterwinter.org, 20 Juni 2018) Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) takribani misikiti yote 436 ili fungwa na kuharibiwa (www.ctvnews.ca, 17 Machi 2015)!

Hakika, Waislamu wanahitaji kwa dharura dola yao ya Kiislamu ya Khilafah ili kuwatunza na kuwasimamia mambo yao dunia kote. Ni hitajio la dharura ambalo ni lazima litimizwe kwa sababu inajulikana kwamba tawala za kisekula ni mabwana katika kupatiliza hali na hivyo wanaweza kupatiliza fursa ya hii ya kuwa njia panda ima kuendelea kufunga au kufungua misikiti nchini Kenya ili kuendeleza ajenda zao ovu za kuwabandikiza Waislamu kuwa wenye misimamo mikali au poa na hatimaye magaidi na kupelekea kutaabishwa zaidi!

Hatua ya kuchukua ni kutafuta suluhisho msingi kwa matatizo mengi yanayokumba Ummah wa Waislamu na dunia kwa ujumla katika kila nyanja ya maisha kuanzia kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu miongoni mwa mengine. Suluhisho msingi ambalo si jingine isipokuwa kusimamisha tena Khilafah ambayo imejaribiwa na kutawala kwa takribani karne 14 kwa huruma na kuwa msimamizi wa amani duniani. Khilafah itahakikisha kwamba sehemu za ibada zikijumuisha zile za raia wasiokuwa Waislamu ziko wazi na zinalindwa wakati wote. Maradhi yanapochipuza idara yake ya afya itahakikisha kuwa raia wote wamelindwa kutokamana na athari na ukali wa maradhi hayo na sera muafaka zitawekwa ili kuhakikisha kwamba maisha ya raia yanalindwa.

Kuchelewa kwetu katika kutafuta suluhisho la kudumu kumetupelekea katika hali yetu hii ya kuwa njia panda ya ima tufungue misikiti yetu kwa mujibu wa masharti ya serikali za kisekula au kuendelea kuifunga!  Njia zote hatimaye hazitatui tatizo. Hii inathibitisha kauli ya Mwenyezi Mungu (swt): وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِڪۡرِى فَإِنَّ لَهُ ۥ مَعِيشَةً۬ ضَنكً۬ا “Na atakaye jiepusha na mawaidha Yangu basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Ta Ha: 124] Na pia, Mtume (saw) aliizungumza hali hii: لَيُنْقَضَنَّ عُرَى الْإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةٌ تَشَبَّثَ النَّاسُ بِالَّتِي تَلِيهَا وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضًا الْحُكْمُ وَآخِرُهُنَّ الصَّلَاةُ “Mafundo ya Uislamu yatafunguliwa moja baada ya jingine, na kila fundo litakapofunguliwa litashikwa jingine, la kwanza kufunguliwa ni Utawala (Khilafah) wa Uislamu; na mwisho litakuwa ni Swala.” [Ahmad na Al-Hakim] Ni lazima tufanye haraka na tuunganishe juhudi zetu katika kuleta mfumo mbadala wa Kiislamu unaohitajika dharura ili kuchukua nafasi ya mfumo uliokufa wa kisekula wa kirasilimali. “«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi (Khalifah) ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda”

 

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir