Jumla

Ngao Yetu

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Khilafah ni yetu ngao, sisi tulo isilamu,

Itatukinga na hao, wamwagao zetu damu,

Ambao kila uchao, huturushia mabomu,

Sisi tulo isilamu, khilafah ni yetu ngao,

 

Khilafah tishio kwao, mabepari madhalimu,

Zina khofu nyoyo zao, inawanyima naumu,

Ufikile mwisho wao, na sasa ndio taimu,

Mabepari madhalimu, khilafah tishio kwao,

 

Khilafah kiboko yao, wahujumu wisilamu,

Kwa chuki zao na mwao, tumwa wanamshatimu,

Hivino vitimbi vyao, vitafikishwa khatimu,

Wahujumu wisilamu, khilafah kiboko yao,

 

Mda huno tulonao, huhalalisha haramu,

Muongozo utungwao, na hawano binadamu,

Huita wauitao, demokrasia tamamu,

Huhalalisha haramu, mda huno tulo nao,

 

Linaabudiwa leo, demokrasia sanamu,

Umefikia upeo, ufisadiwe ni sumu,

Dawa yake ipeteo, ni ya khilafah nidhamu,

Demokrasia sanamu, linaabudiwa leo,

 

Khilafah waipingao, ni finyo zao fahamu,

Hawana huja na bao, kazi yao kutuhumu,

Ndo dola itakiwao, na kila muislamu,

Ni finyo zao fahamu, khilafah waipingao,

 

Khilafah ina mafao, kwa wote wanaadamu,

Wema, adili, mazao, itausha udhalimu,

Fukara waso makao, watamudu kujikimu,

Kwa wote wanaadamu, khilafah ina mafao,

 

Jama khilafah iyao, kwa idhini ya karimu,

Ni bishara ing’arao, kataja tumwa hashimu,

Tuweni wajitumao, ahadi ipatetimu,

Kwa idhini ya karimu, jama khilafah iyao,

 

Mtunzi – Mohammed Bakari

 

Almufti

 

Mombasa – Kisauni