Jumla

Okoa Vijana

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Mabarobaro ni kiungo muhimu sana kwa Ummah wowote ule. Wao ndio uti wa mgongo katika jamii. Na nitegemeo kubwa kwa mafanikio ya mujtama. Wao ndio wenye hima ya juu kutoka na nafsi kuwa tayari kutekelza mambo. Na nguvu ya Ummah huangaliwa kutengenea kwa vijana wake na misimamo yao katika dini yao, uhodari wao na vipaji vyao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى* وَرَبَطْنَا عَلَى قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ لَنْ نَدْعُوَ مِنْ دُونِهِ إِلَهًا لَقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا)

“Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidishia uwongofu. Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mipaka.” [Al-Kahf: 13-14]

Kwa hakika Uislamu umezingatia pakubwa kumchunga barobaro kwa hali ya juu kwa kufanya hima kumuelekeza njia ya sawa. Kwa sababu wao niwepesi kuikubali haki kuikumbtia na kuipenda. Kwani hiki ni kipindi ambacho mwanadamu huwa na nguvu na nishati ya hali ya juu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(اللَّهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ)

“Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya uonyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.” [Ar-Rum: 54]

Vilevile Mtume wetu (saw) alikuwa ana pupa sana na hamu kubwa katika kuwalea vijana akijua kuwa hakika kutumikia Uislamu na Waislamu ni vigumu bila kupata vijana. Na ndio katika moja ya hadithi zake (saw) akasema: na barobaro aliyekulia katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) miongoni mwa watu aina saba watakao pata uvuli wa Mwenyezi Mungu. Na akatuhimiza tupatilize katika mambo matano kabla ya kufikiwa na matano moja wapo ni ujana wetu kabla ya uzee.

Na ili hili lifanikiwe hakuna budi mabarobaro wapate mafundisho sahihi aliyoyaleta bwana Mtume (saw) ili kujenga ufahamu na fikra sahihi. Walelewe kuipenda dini na kuitabikisha na kuubeba ujumbe wa Uislamu ili Uislamu uweze kusonga mbele. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنْ الْمُنكَرِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu.” [Ael-e-Imran: 110]

Vijana wetu wahitaji mno wafahamu wema waliotutangulia kwa juhudi walizotia katika kubeba majukumu na uwajibu wake kwao. Ili waweze kuiga na kuchukua mifano mema kutoka kwao.

Leo thaqafa anayopewa katika taasisi zote za kielimu zimelemaza fikra za mabarobaro. Kukapatikana wale waliozama katika fikra za kigeni wakapotea njia na kupoteza wengine bila kufahamu. Na hili ndilo pote kubwa katika safu za Waislamu waleo. Na pote jengine dogo lenye ghera na hamu kuu ya dini yao pasina muongozo sahihi. Mtume (saw) alikuwa akiomba azidishiwe elimu na aruzukiwe fahamu. Bali elimu bila ya fahamu hupelekea utekelezaji wa kimakosa.

Na kwa kuwa wamagharibi wamesimama kidete kuharibu ummah kwa kuharibu vijana (shababu) wake haina budi sisi kama jamii ya Waislamu kusimama kidete kupambana na mawimbi haya makali.

Ama pote la kwanza lile la vijana waliomeza fikra za demokrasia na uhuru. Hawataki kusikiza nasaha mpaka za wazazi wao. Wakashughulishwa na mitandao na kupuuza vizazi vyao (ulul-arhaam). Wakawekewa michezo na kusahaulishwa swala zao. Wakamsahau Mola na kujipinda kwenye mambo ya anasa na pumbao. Na kila uchao hali yazidi kuwa mbaya. Kwa sababu wamejengwa juu ya uhuru wa kujifanyia atakalo. Mpaka wakahisi kuwa Uislamu unawapa shida katika maisha yao.

Enyi vijana tuzinduke toka usingizi tufahamu ya kuwa Uislamu umekuja kutuwekea njia bora ya kuishi ndani ya huu ulimwengu. Kwa namna ambayo inatuhakikishia furaha ya kikweli hapa duniani na kesho akhera. Mpangilio ambao hauna kasoro unaotokana na Muumba wetu.

Ama pote la pili ni lile liliopotea njia kwa kufuata njia (manhaj) isiyokuwa ya Mtume (saw). Kwa kuwa na ghera ya dhati na dini yao wakabuni fikra zisizotokamana na dini kwa sababu ya ufahamu wa kimakosa. Niwajib tujuwe ya kuwa kufaulu kwetu kupo katika kuifuata njia sahihi ya Mtume (saw) ya kuleta mabadiliko

Na nilazima zaidi wana da’wah wawe na hekima na subira katika kuingiliana/kuamiliana na mabarobaro katika kurekebisha fahamu na tabia zao na iwe kiigizo chao ni Mtume (saw) kwa kuwapa majukumu na kuwanasihi vizuri. Kwani yeye (saw) hakuwa mkali alipojiwa na barobaro kuomba ruhusa akafanye uzinifu. Bali kwa upole yeye (saw) akamueleza madhara yake na kumuombea Mwenyezi Mungu. Ni muhimu pia kujuwa vipawa vya ummah vinavyo ambatana na mafundisho ya kidini na kuvikuza ili kupatikane jamii ya kujitosheleza katika kila nyanja ya maisha iwapo mabadiliko madhubuti yapatikane. Na kutoa wanaume wa kikweli watakao pambana na mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake ovu kwa kuusimamisha Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]

Ali Mohamed Ali

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Kenya