Jumla

Sehemu ya Kwanza: Hali ya Kiuchumi ya Kenya

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Kenya ilipopata “Uhuru Bandia” mwaka 1963 Pato la Taifa (GDP) lilikuwa Dola za Marekani milioni 926.6 ikiwa na idadi ya watu milioni 8.9 ikiwa ni mgao wa Dola za Marekani 104 kwa kila mtu kwa mwaka. Kufikia mwaka 2018 Pato la Taifa lilikuwa ni Dola za Marekani bilioni 85.98 ikiwa na idadi ya watu takribani zaidi ya milioni 48 ikiwa ni mgao wa Dola za Marekani 1,790 kwa kila mtu kwa mwaka. Takwimu zinaonyesha sekta zinazochangia katika ukuaji wa GDP ni sekta ya huduma (biashara za jumla na rejareja, uchukuzi, fedha n.k), sekta ya viwanda na utengenezaji na sekta ya kilimo mtawalia. Kiasi kufikia Jumanne, 30 Septemba 2014, Kenya ilitangazwa kuwa nchi ya 9 Afrika yenye uchumi mkubwa na kupanda daraja na kuwa “Nchi ya Mapato ya Kati” (https://www.brookings.edu, Ijumaa, 3 Oktoba 2014)

Kwa upande mwengine madeni jumla (nje na ndani) yakadiriwa kufika kiwango cha zaidi ya trilioni Ksh7 mwaka 2020. (The East African, 18 Disemba 2018). Huku Bajeti ya trilioni Ksh3 ya mwaka 2018/2019 ilikuwa na pengo la bilioni Ksh500! Ukuaji wa GDP unaashiria kuwa Taifa la Kenya lipo katika njia imara na wakati huo huo kuzidi kwa madeni kuna ashiria kuwa Taifa liko katika mkondo mbaya mno na unaweza kuipelekea nchi hii kusakamwa na madeni kiasi kwamba uchumi wake utasambaratika.

La kushangaza ni kuwa tangu tupate “Uhuru Bandia” pengo kati ya masikini na matajiri linazidi kukuwa tena kwa kasi kubwa. Licha ya uchumi wa Kenya kuwa mkubwa ndani ya eneo la Afrika Mashariki na Kati na Nairobi kuwa ndio kitovu cha biashara za eneo hilo. Raia nchini Kenya wanazama ndani ya Umasikini kwa asilimia 45.9 (https://www.bbc.com, 30 Septemba, 2014). Kwa maana nyingine zaidi ya Wakenya 4 kati ya 10 wanatumia takribani Dola za Marekani 1.90 kukidhi mahitaji yao!

Kenya ni dola kibaraka wa mkoloni Muingereza; kwa hiyo nidhamu yake ya uchumi inatokamana na mfumo wa kisekula wa kirasilimali ambao imeurithi kutoka kwa bwana wao Muingereza. Kwa hivyo daima haitarajiwi kukuwa kwa uchumi kutapelekea kuboresha hali za raia jumla isipokuwa kwa wachache walio katika mduara maalumu ndani ya utawala na wengine wanabakia pembezoni tu! Sera ya nidhamu ya uchumi wa kirasilimali imekitwa katika kulimbikizia matajiri utajiri na kuwalimbikizia umasikini walala hoi! Lakini kwa sharti kwamba walala hoi waendelee kupawa pumzi wasife ili waendelee kuwatumikia matajiri majumbani na viwandani mwao na vijipesa wanavyopewa kupitia mkono wa kulia kama mshahara vinaporwa tena kupitia mkono wa kushoto kwa njia ya ushuru!

Hali hii itaendelea mpaka pale Wanadamu watakapozinduka na kufahamu kuwa tatizo sio uchumi kukuwa polepole au haraka bali ni itikadi ya kisekula ya kutenganisha dini na maisha ndiyo chanzo cha mashaka tuliyonayo ikiwemo asilimia kubwa ya umasikini wa kupindukia! Itikadi hii na mfumo wake wa kirasilimali zimempa mwanadamu majukumu ya kujipangia namna ya kuishi apendavyo ikiwemo kujitungia sheria mwenyewe namna ya kuendesha mambo yake. Nidhamu zake ikiwemo ya kiuchumi inaendeshwa kwa matamanio ya nafsi za watu, kiasi kwamba badala ya serikali kuendea mbio raia wake wapate mahitaji msingi mfano chakula, mavazi na makaazi wao wanakwenda mbio eti “kuwekeza katika miundo mbinu n.k” ili kuukuza uchumi! Ni uchumi gani ambao unalengwa kukuzwa ilhali madeni yanazidi kuwa makubwa na raia takribani asilimia 50 wanashindwa kukidhi mahitaji yao msingi?!

Shiriki Katika Kampeni yetu Maalumu kwa Mwito: Kuzidi Kwa Gahrama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba kwa kufuatilia hashtag hii: #KuzidiKwaGharamaZaMaisha_UislamuNdioTiba napia kwa kuzuru Link zifuatazo

Tovuti: https://hizb.or.ke/sw/2019/01/12/kampeni-maalumu-chini-ya-mwito-kuzidi-kwa-gharama-za-maisha-uislamu-ndio-tiba/

Twitter: twitter.com/HT_KENYA

Tanbihi: Makala Na.29 ifuatayo itaelezea Uchumi wa Kiislamu chini ya Serikali ya Khilafah.

 

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya