Habari na Maoni

Serikali kuongeza hofu nyengine ya njaa baada ya ile ya Virusi vya Corona!

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Kama hatua yake mpya ya kukabiliana na janga la kiulimwengu la Virusi vya Corona, serikali imeamua kuyafunga maeneo mawili yenye idadi kubwa ya Waislamu ambao pia ni vituo muhimu vya kibiashara; Eastleigh Jijini Nairobi na Oldtown Mombasa. Madai ya Serikali kuwa hatua hio haikuchukuliwa kwa nia ya kuadhibu wakaazi wake, bali ni kwa malengo ya kulinda maisha ya wakenya dhidi ya maambukizi, ambavyo inasemekana kwamba maeneo hayo yamerekodi visa vingi vya Covid-19

Hatua hii itaendeleza zaidi hali mbaya ya kiuchumi hasa ikizingatiwa kwamba maeneo hayo hutumiwa na watu wengi katika kuendesha  biashara  kama njia ya kuweza kukimu mahitaji yao kila siku. Hatua ya kuweka vikosi vikubwa vya polisi inaonyesha wazi kwamba marufuku hayo ya kuzuia kuingia na kutoka maeneo hayo kwa siku kumi na tano, ni kuwaadhibu na kuwanyanyasa wakaazi wake kiuchumi. Ni bayana kwamba kwamba serikali imeamua kuongeza hofu nyengine ya njaa kwa raia wake baada ya ile ya maradhi ya Corona. Cha kutamausha ni kwamba vikosi vya usalama vinavyohakikisha marufuku hayo yanatekelezwa, havikuonekana pindi magenge ya vijana yalipokuwa yakitekeleza uhalifu dhidi ya wakaazi wa Old Town. Na huku serikali ikidai kuwa hatua yake hiyo ni kujali maisha ya raia wake, maajabu serikali imepuuza raia wengine walioachwa bila makao kwa sababu ya mafuriko! Linalohuzunisha ni kuwa tokea msimu wa mvua za masika kuanza hadi sasa mafuriko tayari yameua zaidi ya raia 100!

Tunasema kuwa, serikali za Kibepari hufadhilisha zaidi masuala ya kiuchumi kuliko yale ya kiafya,wakuu wa serikali ya Kenya waliruhusu ndege kutoka China kutua humu nchini baada ya mkurupuko wa maradhi ya Corona huko China. Na sasa kinaochonekanwa ni kwamba serikali inacheza mchezo wa kuwatupia lawama raia wake ilhali iliruhusu virusi hivyo kuingia nchini.

Suala la upimaji ili kujua maradhi ni jambo zuri, ila hatua ya raia kususia zoezi hili inamaanisha kwamba hawana imani na viongozi ambao wamekuwa na mazoea ya kuhadaa raia kila siku. Mifumo duni ya Kiafya na takriban huduma zote za Kijamii yote haya yamefanya raia kutokuwa na imani na Serikali. Tayari kuna ripoti kwenye baadhi ya vyombo vya habari zikionesha baadhi ya watu waliowekwa kwenye karantini za serikali wakitoroka na wengine kutishia kujitoa uhai wao kwa sababu ya shida wanazokumbana nazo.

Kwa ujumla maradhi ya Corona yametuonyesha kwamba jamii ya Kenya bali ulimwengu kwa ujumla imekosa usimamizi wa  kikweli wa mambo yao. Na kwamba viongozi wa kisekular kote duniani hubwagia lawama na kutisha raia wao kama njia moja wapo ya kujaribu kuficha utepetevu wao wa kila mara. Hivyo kuna haja kubwa sana ya umma kote duniani kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir  kuleta uongozi unaojali kweli maisha ya watu sio kwa misemo tu bali kwa vitendo. Uongozi huo sio mwengine bali ni Khilafah ambao kiongozi wake hatochukulia utawala kama chombo cha kunyanyasa raia wake kwani atafahamu kwamba kuna siku ataletwa mbele ya mfalme wa wafalme aulizwe jinsi gani alivyosimamia raia wake. Serikali hiyo ni Khilafah chini ya njia ya Bwana Mtume SAAW ambayo kikweli raia ndio watakua na imani nayo.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut Tahrir in Kenya

 

REF: 1441/10AH,

Saturday 16th Ramadhan 1441AH/

09/05/2020 CE