Habari na Maoni

Serikali za Kisekula Zimebadilisha Majanga ya Kimaumbile kuwa Mgogoro

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Habari:

Wiki kadhaa zilizopita mvua nyingi iliweza kunyesha nchini na vyombo vya habari vimeripoti kuzidi kwa hali mbaya na vifo nchini kote ikijumuisha maeneo ya Kati, Pwani na Kaskazini mashariki huku wajuzi wakitoa ilani ya kukithiri kwa hali mbaya. Tukio la hatari zaidi la hivi majuzi ni kufariki kwa watu 50 huko Pokot Magharibi kutokana na mafuriko yaliyo haribu nyumba na kusababisha maporomoko ambayo yaliwazika wakaazi, kwani lililkuwa tukio hatari zaidi la kimaumbile ndani ya miaka ya hivi karibuni.

Maoni:

Mvua zimefichua kwa mara nyingine Serikali za Kisekula kukosa uwezo wa kusimamia majanga. Vifo vya huko Pokot Magharibi vingelipunguzwa kwa kuwepo maandalizi ya mikasa. Ni jambo la kushangaza kwamba siku kadhaa baada ya mkasa huo watu hawajaweza kuhesabiwa na hivyo kudaiwa kuwa wamekufa. Lakusikitisha zaidi maafisa wakuu serikalini wakiongozwa na Waziri wa Ndani Fred Matiang’i hawakuweza kufika katika kijiji ambako watu waliweza kufariki kinyama. Hali isingelifikia kiwango hicho lau serikali ingelikuwa imejiandaa na kuchukua hatua za mapema.

Kutokana na kukosekana sera ya nyumba za serikali na uporaji wa ardhi kutoka kwa maafisa wa serikali; familia nyingi masikini zimejipata hazina ardhi salama za kuishi na hivyo kuhatarisha maisha yao kwa kujenga katika sehemu ambazo zina mafuriko. Mpangilio mbaya wa barabara hususan katika maeneo ya ndani ndani hazijengwi kudumu kwa sababu ya ufisadi ambao umewafanya watu asilimia 32 kuishi katika maeno yaliyo na kilomita mbili za barabara za msimu na hili linazidisha hali mbaya wakati mafuriko yanapotokea kwa kuwa waathiriwa huwa hawana lakufanya.

Janga hili kiuwazi linaonyesha namna tawala za kirasilimali zinavyo badilisha mikasa na kuwa migogoro ya kibinadamu. Aghalabu mara nyingi mikasa hiyo inapotokea, inadhihirisha umbile la kweli la urasilimali na nidhamu zake tawala ambazo hazipeani kipaumbele kwa maslahi ya umma. Katika kinyang’anyiro cha uongozi, wanasiasa masekula warasilimali huzurura nchi yote kwa ndege wakitafuta kura lakini wakati wa mafuriko wanatizama kupitia runinga ilhali umma unazama! Hiyo ndiyo sura kamili ya urasilimali na viongozi wake ambao wanathamini tu maisha yao na hawayapi umuhimu maisha ya walalahoi.

Hata kama ni kweli mwanadamu hawezi kuzuia mikasa ya kimaumbile, lakini Mwenyezi Mungu (swt) amemuamrisha mwanadamu huyo kuchukua tahadhari za mapema kwa kuweka mipango kabambe kama njia ya kupunguza athari ya mikasa itakayotokea. Kama nidhamu kamili, Uislamu unaliweka jukumu la kusimamia mambo ya umma kwa serikali na sio watu binafsi. Mtume (saw) alisema:   «الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»“Kiongozi wa watu ni mchungaji na atahesabiwa juu ya raia wake.”

Dola ya Kiislamu, al-Khilafah imepewa jukumu la kuhifadhi maisha ya raia wake wakati wote. Ama kuhusiana na mikasa kama mafuriko na maporomoko, Khilafah itatumia fedha zilizoko katika hazina (Baitul Mal) ili kuwasimamia walioathirika na jukumu lake juu kwa umma sio fadhla. Lau itakuwa hakuna fedha katika hazina, basi Khalifah atalazimika kuwatoza matajiri kiwango maalumu cha kodi ili kutatua tatizo hilo. Hivi ndivyo Khilafah inavyotarajiwa kuyalinda maisha adhimu ya raia wake bi idhni llah Taala.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya