Taarifa za Eneo

Siasa za Chuki na Migawanyiko ni Dalili Tosha ya Kufilisika Kifikra kwa Siasa ya Demokrasia na Wafuasi Wake

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Hatimaye, rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili kwenye sherehe iliohudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali na kususiwa na wanasiasa wa upinzani. Hafla hii imekuja huku nchi ikighubikwa na migawanyiko ya kikabila, semi za chuki na umwagikaji wa damu. Kwenye hotuba yake rais Kenyatta amekiri kuwa anakabiliwa hapo mbeleni na kazi ngumu ya kuleta uwiano na kuunganisha taifa lililogawanyika na ambalo hujipata kwenye shimo la taharuki kila wakati wa uchaguzi.

Sisi Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kusema yafuatayo:

Matatatizo ya migawanyiko ya kikabila, taharuki na mauaji yanayoshuhudiwa katika misimu ya uchaguzi hayo yote yanafichua kufilisika kifikra kwa wanasiasa wa Kidemokrasia kiasi cha kuwa kampeni zao hujikita katika kuibua chuki na mitafaruku baina ya raia.  Na hili sio kwa wanasiasa wa Kenya bali hata kwa mataifa ya magharibi kama tunavyoona kampeni ya chaguzi zao jinsi wanavyochochea chuki kati ya Waislamu na Wakristo, baina ya watu weupe na weusi. Yote haya ni dalili  wazi sasa wanakubali kuwa hawawezi kushinda kura kwa kuegemea sera zao  mbovu za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Isitoshe ni kuthibitisha kutojimudu kwa mfumo katika kuondoa matatizo ya migawanyiko ya kikabila.

Ni kweli kuwa matatizo ya Kenya yanahitaji kutatutiliwa lakini kwa kuwa wanasiasa wa mirengo yote ima walioko katika utawala au upinzani wote wamekumbatia  sera mbovu za mfumo wa kibepari wa Kirasilimali ambao ndio chanzo halisi cha matatizo yote yanayoikumba Kenya na ulimwengu kwa ujumla.  Mfumo wa kibepari umejengwa juu ya kumtajirisha tajiri kwa kumnyonya mlalahoi hatimaye kukuza mwanya mkubwa baina ya mabwenyenye na walalahoi. Na hii ndiyo sababu iliopelekea serikali tatu zilizotawala Kenya kushindwa kutatua matatizo ya raia licha ya kufanyika marekebisho kadhaa ikiwemo kubadilishwa kwa katiba na kamati za uchaguzi. Hivyo matakwa ya upinzani kutaka merekebisho ya mfumo wa uchaguzi, kuheshimu utawala wa sheria yote hayo ni  kujaribu kupaka rangi mfumo ulio na msingi muovu.

Tunasema Kenya na ulimwengu jumla inahitaji Uislamu ulio na muundo mzuri wa Kisiasa (Khilafah) utakao kuwa na suluhisho kwa matatizo ya wanadamu wote. Uislamu hufasiri siasa kuwa ni kusimamia kwa dhati mambo ya watu wala sio ung’ang’anizi wa utawala baina ya wanasiasa kufikia manufaa yao ya kibinafsi. Nidhamu ambayo vyama vya kisiasa ndani yake vitakua sio vyombo vya kufikia tu madaraka bali kuihesabu serikali ili iweze kutimiza majukumu yake kwa raia kikamilifu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 02 / 1439 AH

Jumanne, 10 Rabiul-Awwal 1439 H

28/11/2017 M

 

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke