Jumla

Suluhisho la Matatizo yanayoikumba Sekta ya Elimu halipo katika Uvaaji wa Sare Sawia bali lipo katika Kuiondosha Sera ya Elimu ya Kisekula ya Kikoloni

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Wakenya wameachwa njia panda kutokana na kauli kinzani baina ya Viongozi katika Wizara ya Elimu na Muungano wa Wazazi (KPA) nchini Kenya kuhusiana na pendekezo la Muungano wa Wazazi Kenya kuwa wanafunzi wa shule za msingi wote kuvaa sare sawia yenye rangi ya kijivu na shule za upili kuvaa sare sawia yenye rangi ya samawati tofauti ikiwa ni alama ya shule pekee. Mwenyekiti wa Muungano huo, Nicholas Maiyo amesema walitoa mapendekezo hayo kwa Wizara ya Elimu kama wazazi baada ya Warsha ya wiki moja iliyoandaliwa huko Machakos mwanzoni mwa Julai, 2018.

Mapendekezo hayo yaliwekwa wazi na Katibu katika Wizara ya Elimu, Belio Kipsang alipokuwa katika sherehe ya kuadhimisha utekelezaji wa mpango wa kukiboresha kiwanda cha nguo kinachomilikiwa na Chuo Kikuu cha Moi; Jumamosi, 7 Julai 2018. Alisema kwamba, Wizara yake inaifanyiakazi sera itakayojumuisha pendekezo hilo la wazazi. “Pendekezo hilo lilitoka kwa wazazi ambao wamekuwa wakilalamika kutokana na gharama ya juu ya ununuzi wa sare za shule…” akaendelea kusema, “Tunataka kuwalinda watoto wetu dhidi ya wale wanao wanyemelea …” akaongezea “Tunapokaribia kuwa na sare sawia katika shule zetu, tunataka Rivatex kujiandaa ili kuweza kucheza dori katika utengenezaji wa sare zitakazohitajika.” Matamshi hayo yalizusha taharuki na gumzo katika mitandao ya kijamii. Siku ya Jumatatu, 10 Julai 2018; Waziri wa Elimu Amina Mohamed alisema kuwa uamuzi wa shule kuvaa sare sawia bado hauja amuliwa rasmi. Akizungumza na vyombo vya habari Jogoo House alitamka “Shule zina wadhamini na hiyo inamaanisha kuwa tuwatake ushauri kabla kufanya maamuzi yoyote.”

Kauli hizi zinaashiria wazi kuwa Serikali haijali sekta ya elimu isipokuwa inajali kunyanyua uchumi wake ambao kihalisia ni kwa tabaka dogo la wanasiasa walafi wa kibepari. Uchumi unataka kuboreshwa kupitia Sekta ya Viwanda chini ya madai ya  kutimiza ruwaza yake maarufu ya Ajenda Nne Kuu (Big Four Agenda). Kwa mujibu wa taarifa ya sera ya makadirio ya bajeti ya 2018 (2018 Budget Policy Statement) iliyotolewa 19 Januari 2018; serikali inapania kuongeza mgao wa mapato ya sekta ya utengenezaji kutoka asilimia 9 hadi asilimia 15 ya uzalishaji jumla wa taifa (GDP) kufikia mwaka 2022.  Kwa upande wa utengenezaji nguo, serikali inalenga kukuza uzalishaji wa pamba kutumia njia za kisasa, ambazo zitakuwa na uwezo wa kuzalisha mara tatu zaidi na kuwapa motisha wawekezaji kujenga mitambo ya nguo madhubuti. Hivyo kupelekea idadi ya 50,000 ya vijana na wanawake kuweza kuhusishwa na sekta hiyo kupitia mafunzo na hatimaye kiwango cha viwanda vya urefu wa milioni 5 kwa mguu kubuniwa kupitia uzalishaji wa pamba. Kwa kufanya hayo sera hiyo inasema ‘Kenya itaongeza mapato kutoka katika sekta ya nguo kutoka bilioni Ksh.3.5 hadi Trilioni Ksh.2, na kutoa nafasi za kazi 500,000 katika kukuza pamba na nafasi za kazi 100,000 katika kutengeneza nguo mpya kufikia mwaka 2022.’

Ni wazi kwamba Muungano wa Wazazi Kenya (KPA) hauna uchungu na hali ya sekta ya elimu kwa kuwa imejisalimisha na kuwa mkono wa serikali katika kuitumikia kufanikisha malengo yake. La msingi ambalo Muungano wa Wazazi Kenya lingekuwa lina washughulisha usiku na mchana ni namna gani wangeliweza kutafuta njia ya kuiondosha sera ya elimu inayotoa dira juu ya elimu ya watoto wao jumla kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Kwa sababu sera ya elimu iliyopo ni ile iliyoasisiwa na mkoloni tangu alipowasili nchini hapa. Nayo ni kuwa Elimu ni ala inayotumika kumakinisha fikra na fahamu za utumwa/kujisalimisha kwa mwanadamu/mkoloni na kufanya vile anavyokuamrisha kwa mujibu wa akili yake inavyomtuma ima umfanyie kazi kiwandani kwake au mahali popote pale. Sera hii imewafanya watoto wakienzi na kutamani kuwa kama wamagharibi wakoloni walio watawala mababu zao. Hili limewapelekea kujisalimisha kikamilifu na kujihisi madhaifu mbele ya maamrisho ya wamagharibi wakoloni wasekula wakirasilimali.

Sera hii iliyoasisiwa juu ya akili finyu ya wakoloni wamagharibi wenye itikadi ya kisekula na mfumo wa kirasilimali haina natija yoyote isipokuwa kuzalisha watumwa wa fikra za kimagharibi zinazopelekea wao kudidimia zaidi ya wanyama kutokana na kuwa fikra hizo ni kinyume na maumbile ya mwanadamu. Mfano mtu ni Professa au Daktari kisha anajienzi kwa kuwa yeye ni ‘Shoga’. Hilo ni jambo lakustaajabisha maanake msomi ni yule ambaye jamii inamtegemea katika kuongoza kizazi kijacho kwa kuwa mstari wa mbele katika upeo wa hali ya juu ya ufahamu. Lakini yeye msomi ndiye aliyekuwa duni thamani; Je huyo mwanafunzi wake atakuwa vipi?!

Suluhisho lipo katika Uislamu; mfumo unaotoka kwa Muumba wa Wanadamu na anayetambua lipi zuri na baya kwa viumbe vyake. Uislamu kupitia Dola ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume, itikadi ya Kiislamu ndio msingi ambao juu yake imejengwa sera ya elimu. Mtaala wa elimu na mbinu za ufundishaji zote zimeundwa kukinga kupotoka kutokana na msingi huu. Lengo la elimu ni kuzalisha shakhsiyya ‘utambulisho’ ya Kiislamu katika fikra na tabia, na kuwapa watu mafunzo ya kisayansi na maisha jumla. Kwa hiyo masomo yote katika mtaala wa elimu yatafunzwa kwa mujibu wa msingi huo.

Ama kuhusu suala la uvaaji wa Sare au Sare sawia hilo sio suala nyeti na halitokuwa na mvutano kama inavyoshuhudiwa hivi sasa nchini Kenya kutokana na kuwa kila mmoja anavutia mrengo wake ili aweze kupata bahashishi zaidi kumliko mwenzie. Kwani Dola ya Khilafah kupitia Khalifah mchajiMungu itatoa muongozo rasmi ulio ndani ya mipaka ya Kishari’ah na unaolenga kuwafanyia wepesi raia watakaokuwa wanaishi ndani ya Dola hiyo wakati huo kuhusiana na wanafunzi kuvaa sare au la.

Kwa mara nyingine imedhihirika wazi kuwa itikadi ya Kisekula na mfumo wake wa Kirasilimali unamtizama mwanadamu kama mashine na daima unaomuangalia kwa kipimo cha faida anachotoa au atakavyotumiwa kufikia uzalishaji zaidi wa viwango vya juu vya taifa au hata kutumika kuhalalisha na kuharamisha mipango fiche ya serikali za kikoloni za kisekula.

Imeandikwa kwa Ajili ya Tovuti ya Radio Rahma

Ali Nassoro Ali

Mwanachama Katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Makala Na.2   Tarehe: Ijumaa, 29 Shawwal 1439 | 2018/07/11

  1. https://www.standardmedia.co.ke/article/2001287257/parents-propose-to-have-all-students-wear-same-uniform
  2. https://allafrica.com/stories/201807100061.html
  3. http://www.treasury.go.ke/component/jdownloads/category/195-budget-policy-statement.html?Itemid=-1
  4. https://www.nation.co.ke/news/politics/How-Uhuru-hopes-to-achieve-Big-Four-agenda/1064-4275586-rdf4pq/index.html