Taarifa za Eneo

Tangazo la Kifo cha mmoja ya walinganizi wa Kiislamu Kenya

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa vyombo vya Habari

(إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutaregea.”

Kwa nyoyo zenye kuamini Qadhaa ya Mwenyezi Mungu, harakati ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir /Kenya, inawatangazia Ummah wa Kiislamu wote kwa ujumla na hasa Waislamu nchini Kenya;

Abdallah Boga (Mola amrehemu) alipatwa na mauti Jumanne, 10 Septemba 2019.

Licha ya kuwa na umri mkubwa Boga alijiunga na Hizb ut Tahrir – chama Kiislamu cha kiulimwengu cha kimfumo ambacho kinalingania kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Mtume (saw). Maradhi yake hayakumregesha nyuma kutotekeleza jukumu lake na wala hatusifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Kwa hakika nyoyo zetu zimejaa huzuni na macho yakitoa machozi kwa kuondokewa na baba na ndugu yetu, twamuomba Mola amsamehe na amrehemu. Ewe Mwenyezi Mungu twakuomba ukirimu mashukio yake na kukunjua kaburi lake.

Hatimaye, tunaipa pole familia ya marhum na kuiombea kwa Mwenyezi Mungu muweza awape moyo wenye kusubiri na kuwalipa ujira na utulivu wakati huu wa huzuni. Twamuomba Mwenyezi Mungu kumbadilishia nyumba bora na familia bora na kutukusanya sisi pamoja naye chini ya bendera ya Mtume (saw) Siku ya Kiyama.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 1441 / 01

Jumatano, 12, Muharram 1441 H

11/09/2019 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke