Taarifa za Eneo

Tangazo la Kifo cha mmoja ya walinganizi wa Kiislamu Kenya

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 (َلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

Na Tutakutien katika misukosuko wa (baadhi ya mambo haya) hofu , njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri . Ambao uwapatapo msiba husema: ‘Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu, na Kwake Yeye tutarejea

[Al-Baqara: 155-156]

Kwa nyoyo zenye kuamini Qadhaa ya MwenyeziMungu na Qadar yake harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Kenya, inawatangazia umma wa Kiislamu wote kwa ujumla na hasa Waislamu nchini kenya kifo cha

Abdallah Ismail (Mola Amrehemu)

Ndugu yetu Mola amrehemu, alikuwa mmoja wa wanachama shupavu wa Hizb ut-Tahrir akibeba ulinganizi wa haki wa kuregesha maisha ya Kiislamu kupitia kuisimamisha tena Khilafah kwa manhaj ya Mtume (saw); na wala hatumsifii MwenyeziMungu yoyote yule.  Alipatwa na mauti Ijumaa asubuhi tarehe 6 Aprili, 2018 sawa na 19 Rajab 1439H baada ya kuugua kwa muda mfupi

Kwa hakika wanaume wa kikweli hufariki lakini misimamo na matendo yao hubakia dira na nuru ya watakao kuja baada yao.

Tunaipa pole familia ya marhum na kuiombea kwa Allah awape moyo wenye kusubiri na kuwalipa kwa ujira wao In Shaa Allah wakati huu wa huzuni. Nasi hatuna la kusema ila lile analoridhia Mola wetu

Kwa hakika nyoyo zetu zimejaa huzuni na macho yakitoa machozi kwa kuondokewa na ndugu yetu,twamuomba Mola amsamehe na kumrehemu na kumweka mahala pema peponi. Ewe Allah twakuomba ukirimu mashukio yake na kukunjua kaburi lake na umpe nyumba bora zaidi kuliko aliyokuwa nayo duniani na nasi tukawe naye chini ya bendera ya Mtume (saw) siku ya Qiyama.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

 

KUMB: 07 / 1439 AH

Jumapili, 21 Rajab 1439 AH/

08/04/2018 M

 

Simu: 0707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke