Tawala kandamizi na Vyombo vya Habari Fisadi ni pacha walioko ndani ya mduara wa Dhulma

Habari  na Maoni

 Habari

Mamlaka nchini Ethiopia imewakamata  Wanahabari wasiopungua 19 wiki iliopita kwa kwa kile kilichotajwa na wanaharakati wa haki za kibinadamu kama “ukandamizaji  wa hivi punde zaidi dhidi ya wanahabari na mashirika huru ya habari unaotamausha na usio na kifani”. Hatua hii ilianza tarehe 19 mwezi Mei pale serikali ilipowazuia korokoni waandishi na wafanyakazi wengine wa vyombo habari takriban 11 katika jimbo la Amhara na la lile mji mkuu wa Addis Ababa. Miongoni mwa aliekamatwa ni Temesgen Desalegn mwanahabari maarufu  mhariri wa Jarida la Fitih, linaloandikwa kwa lugha ya Amharic. Chanzo: [Nation Media Group]

Maoni:

Kamatakamata hii ya wanahabari, wanaharakati na wakosoaji wengine imekuja siku chache baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kusisitiza mnamo tarehe 20 mwezi Mei, haja kubwa ya kuweko na oparesheni za polisi” kwa kile alichosema hatua hiyo ilikuwa ni kulinda raia na kuhakikishia utulivu wa taifa”. Wiki iliopita maofisaa wa usalama katika eneo la Amhara walitangaza kushikwa kwa watu 4500 kama oparesheni kubwa ya polisi.

Ethiopia imekuwa ikipata shutma kote duniani kwa kutozingatia kanuni za kimataifa za uhuru wa kujieleza wa vyombo vya habari. Jumane tarehe 24, Mei 2022 Amerika ilipiga kelele kwa serikali ya Ethiopia juu ya kamatakamata yake ya wanahabari. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price alipongeza zoezi la usitishwaji wa vita na hatua ya kutuma misaada ya kibinadamu katika eneo liloathiriwa na vita la kaskazini mwa nchi lakini pia akatoa mwito kwa serikali kulinda uhuru wa wanahabari mtandaoni na nje ya mtandao.

Hakuna la kustaajabisha kuwa serikali za Kibepari za Kisekula hutumia mbinu zozote zile kunyamazisha wale wote wanaofichua maovu yake hata kama ni kukiukwa miito hiyo inayoitwa uhuru wa uanahabari. Kinaya ni kwamba wanasiasa wa Kimagharibi ambao huja katika safu ya kwanza kushtumu kwa kuwalaumu mawakala wao kote Afrika na ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuwaambia kuwa wanahujumu uhuru wa waandishi wa habari utawaona wako kimya pale utawala muovu wa umbo la kiyahudi unapofanya maovu. Utawala wa Ethiopia bali  Afrika kwa ujumla,wameonesha na kuwakilisha  sura ya maovu ya mataifa ya kimagharibi kama vile Marekani,ambayo inashiriki katika kuibua  vita kupitia utawala muovu wa Abiy Ahmed.

Kwa kile kiambiwacho uhuru wa wanahabari ambao ni mojawapo ya misingi ya Jamii ya Kidemokrasia,hivyo huruhusiwa watu kutafuta habari na kuzisambaza, kuhabarishwa, kuwa na fikra, rai na maoni, pia kuwajibisha viongozi. Ingawa yote haya katika Jamii ya Kidemokrasia hayako hivyo kwani miito ya uhuru na misingi hii hukiukwa. Uhuru wa wanahabari au uhuru wa kujieleza hutiliwa mkazo tu pale unapoafikiana na matakwa ya serikali la sivyo chochote dhidi ya serikali katu hakivumiliwi bali hukabiliwa kwa ukali vilivyo. Kwa upande mwengine aidha, serikali za Kidemokrasia hukejeli na kutukana Uislamu chini ya vazi hilo hilo la uhuru wa wanahabari! Bali wanahabari wamekuwa wakitusi matukufu ya Uislamu huku walindwa na serikali hizo hizo.

Inabainishwa katika kifungu 103 cha mswada wa katiba ambayo Hizb ut-Tahrir ilichukua na kuipeana kwa umma:  Taasisi ya Ofisi ya Habari inakua na kazi ya kurasimu na kutekeleza mikakati ya kisiasa ya vya vyombo vya habari  vya serikali ili iweze kuafiki maslahi ya Uislamu na Waislamu. Ndani ya serikali, taasisi hii inafanya kazi ya kujenga jamii ya Kiislamu iwe imara na yenye utangamano na kuepusha chochote katika mawazo mabaya huku ikisisitiza maadili mema. Katika masuala ya nje ya nchi mkakati huu umejikita katika kueneza Uislamu katika kipindi cha amani na vita kwa namna ya kueleza utukufu wa Uislamu uadilifu wake,nguvu ya jeshi lake huku ikifichua ufisadi  na ukandamizaji wa tawala za kibinidamu  udhaifu wa   jeshi lake. Kwa ujumla kifungu hiki kinaweka sera ya habari na usimamizi wake. Maudhui na habari za vyombo vya habari lazima yawe na ustawi mkubwa wa kiakhlaq, kujenga ufahamu, udadisi wa kisiasa, na uwezo wa kuunganisha habari kwa kuzitumia kwa njia inayohitajika. Vyombo vya habari lazima viwe na maadili ya kazi na kuwa na sifa nzuri ya kiutendakazi inayopelekea raia kuwa na usalama na amani.

Hii kwa uhakika ndio mantiki ya sera halisi ya vyombo vya habari ambayo kwayo Khilafah kwa mfumo wa Utume tutashuhudia vyombo hivi vitaeneza habari kiuadilifu na uaminifu, kuchukulia masuala ya umma na kuweza kupoza vifua vyetu kutokana na tawala mbovu na vyombo vya habari vyenye upendeleo.

Imeandikwa kwa Ajil ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir ,Kenya

31/05/2022.

 

 

Comments are closed.