Tunapongeza Umma wa Kiislamu kuingia  Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut- Tahrir Kenya kwa furaha inatuma salamu za pongezi kwa Waislamu nchini na kote ulimwenguni kwa ujuma kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Tunapoingia kwenye mwezi huu wa  Rahma, Msamaha na kuachwa huru na moto, tunamuomba MwenyeziMungu Swt atupe nguvu na afya za kutelekeza ibada tukufu ya swaum ambao sio faradhi tu bali pia ni moja wapo ya nguzo tano za Uislamu

MwenyeziMungu Subhaanahu wa Ta’ala ameufanya uchaMungu kuwa ndio lengo hasa katika ibada hii tukufu. Uchamungu ndio msingi wa utambulisho wa Kiislamu unaopaswa kudhihirika na kuonekanwa katika matendo yote ya waumini katika kutekeleza maamrisho ya MwenyeziMungu na makatazo yake. Na ili jamii nzima iweze kuwa na uchaji Mungu kunahitajika dola inayowajibika katika kutekeleza Uislamu katika nyanja zote za maisha. Tunaeleza bayana kwamba dola hii sio nyengine bali ni Khilafah ambayo kwa idhni ya MwenyeziMungu itasimamishwa katika moja wapo ya nchi za Kiislamu.

Jamii ya Kiislamu inapoingia katika mwezi huu uliobarikiwa, bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia, mafuta, unga wa ngano, sukari ni ghali sana. Huku wananchi wakiendelea kuteseka na wengine kufariki kutokana na njaa kali katika baadhi ya maeneo nchini, wanasiasa wa mirengo yote ya kisiasa wamejikita katika kampeni za domo kaya kujitafatua vyeo huku wakiwaahidi  Wakenya maskini ahadi tupu! Hili linafaa kuwa ukumbusho tosha kwa jamii ya Kenya kwamba uongozi wa kibepari haujali maslahi ya raia wake.

Ingawa vita vya Ukraine vimeathiri uchumi wa dunia kwa kiasi fulani kwa kuzingatia hali ya soko ya bei ya mafuta duniani kwani  vita hivi  vinazunguka mataifa yanayoongoza, hii hata hivyo, sio sababu kuu kabisa ya mfumuko wa bei wa sasa wa kimataifa. Mfumo wa uchumi wa kibepari umefanya bei kuwa msingi wa uzalishaji na usambazaji wa mali. Zaidi ya hayo, Mfumo hutumia sera ya fedha za makaratasi  bila thamani ya ndani katika sarafu yake kuifanya iwe ya kupunguka kwa bei kila mara.

Twamoumba MwenyeziMungu SWT atakabali amali zetu na kuupa Umma huu mlinzi na kinga halisii nayo ni Khilafah kwa mfumo wa Utume . Khilafah ndio kwa mara nyengine tena itawanasua wanadamu kutoka majanga haya ya Kiuchumi.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya

Comments are closed.