Jumla

Uchaguzi wa 2020 wa Malawi: Ushindi kwa Mfumo Batili wa Kisekula wa Kirasilimali

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wamalawi walishiriki uchaguzi mnamo 21 Mei 2020 ambao Peter Mutharika wa chama cha DPP alishinda kwa kura asilimia 38.6 na mnamo 3 Februari 2020 mahakama ya kikatiba ikafutilia mbali Uchaguzi wa 2019 na kuhukumu kwamba Peter Mutharika hakuchaguliwa sahihi kama raisi. Kwa kuongezea ikaamrisha uchaguzi urudiwe tena ndani ya siku 150. Maamuzi ya mahakama yalitokana na makosa “yakinidhamu na yaliyoenea” (www.ibtimes.com, 04/07/2020).

Kwa hiyo uchaguzi wa marudio ulifanyika mnamo 23 Juni 2020 na Lazarus Chakwera wa chama cha MCP alitangazwa kuwa mshindi kwa kura asilimia 58.5. Majibu hayo yaliifanya Malawi kuingia katika historia kama nchi ya kwanza kwa chama cha upinzani kumng’atua rais aliyeko mamlakani baada ya uchaguzi wa marudio uliosababishwa na kubatilishwa.

Ni muhimu kuzingatia kwamba katika dunia hii inayotawaliwa na mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu yake ya usimamizi yenye sumu ya demokrasia; uchaguzi sio chochote bali ni mazoezi ya kimasudi na kujirudiarudia yanayotumika kuwadanganya na kuwalaza watu wanaodai mabadiliko duniani. Kwa kuwa walioko mamlakani wanafahamu fika kwamba chochote kile ambacho hakilengi kung’oa na kubadilisha mpangilio uliopo wa kisekula duniani SIO tishio kwao na hivyo kushinda au kutoshinda kura sio tishio la kimsingi kwa hali iliyopo. Hivyo basi kushinda kwa Lazarus Chakwera kupo ndani ya mzunguko wa sumu wa kisiasa uliochorwa na Wamagharibi wakoloni mabwana ambao ndio walinzi wa mpangilio wa kisekula wa kirasilimali duniani wakiongozwa na Amerika na washirika wake. Watu wanatumika kama ngazi za kisiasa na wanasiasa masekula ili kuingia au kubakia mamlakani kwa ajili ya kutumikia maslahi yao binafsi na mabwana zao! Dini hutumika kuzipatiliza hisia na baada ya kutimiza malengo inabakia pembezoni kwa mujibu wa itikadi ya kisekula.

Ili kuthibitisha hilo, kabla hata kile kinachoitwa vumbi la mageuzi kutulia tayari watu wanamkashifu Chakwera kwa kupigia debe upendeleo na uajiri wa wapambe ndani ya serikali. Kutokana na uteuzi wake katika baraza hivi karibuni ambako kuliwahusisha watu wa karibu na wengi kutoka Eneo la Kati anakotoka. Kukashifu huko kunaongozwa na wataalamu na watu mashuhuri ambao wanasema kwamba rais kwa “haraka amejigeuza na kuwa muuzaji mzuri wa maneno na balagha huku akiwaandalia wa Malawi chakula kilichovunda ambacho wamekila kwa miaka 26” (aljazeera.com, 09/07/2020).

Hiyo ndiyo hali ya mfumo wa kirasilimali na nidhamu yake yenye sumu ya kidemokrasia inavyowahadaa watu kwamba inawatatulia matatizo yao lakini ndiyo sababu msingi iliyopenyeza katika nyanja za maisha kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo basi, kupelekea kuenea kwa umasikini, kuzidi kwa pengo kati ya masikini na matajiri na kudunisha utukufu wa uhai wa mwanadamu. Kubadilisha wanasiasa sio suluhisho badala yake kubadilisha mfumo na nidhamu zake zinazochipuza kutoka kwake ndio muelekeo sahihi.

Dhati ya ukombozi wa kweli ipo katika kuung’oa na kuubadilisha mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake ovu kwa mfumo wa Kiislamu unaotoka kwa Muumba wa mwanadamu na Mpangiliaji wa maisha ya mwanadamu. Kuukumbatia mfumo wa Uislamu na nidhamu zake kutakata mahusiano ya wakoloni na watawala vibaraka ambao wanafuja rasilimali za Afrika kwa maslahi yao na kuwatokomeza wenyeji katika umasikini. Nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu itaondosha mikopo ya riba na ushuru ili kuwahakikishia watu maendeleo na ustawi wa kweli. Hayo yanaweza kutimia pale watu watakapoamua kuachana na mfumo wa kisekula wa kirasilimali. Kinyume chake watu wa Malawi na duniani kote wataendelea kushiriki katika uchaguzi wa kujirudiarudia ambao hautawanusuru kutoka katika majanga yanayo wakumba hivi sasa!

Ali Nassoro Ali