Jumla

Ulinganisho wa Nidhamu ya Kiuchumi ya Kiislamu (Khilafah) na Kirasilimali

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Na. Nidhamu ya Uchumi wa Kiislamu (Khilafah) Nidhamu ya Uchumi wa Kirasilimali (Kenya, Marekani n.k)
1. Inatokana na Shari’ah (Qur’an na Sunnah) Inatokana na Usekula (Kutenganisha dini na maisha)
2. Mtu Hana Uhuru wa Kumiliki –Kipimo ni Halali na Haramu Mtu Ana Uhuru wa Kumiliki –Kipimo ni Faida na Hasara
3. Tatizo la Kiuchumi ni Usambazaji wa Mali Tatizo la Kiuchumi ni Uchache wa Bidhaa na Huduma
4. Sera ya Kiuchumi iko kuhakikisha raia wanadhaminiwa mahitaji yao msingi ya kibinafsi (chakula, mavazi na makaazi) na kimujtaa (usalama, elimu na afya) na kuwawezesha kupata mahitaji ya ziada Sera ya Kiuchumi ipo kuhakikisha viwanda vinazalisha bidhaa na huduma kwa wingi. Viwanda vinawezeshwa kwa kuondoshewa/kupunguziwa ushuru, kodi na kupewa mikopo ili viendelee kuzalisha.
5. Sarafu ya matumizi ni dhahabu na fedha au Pesa za Makaratasi yaliyo na thamani kwa mujibu wa dhahabu na fedha Sarafu ya matumizi ni dola ya marekani na Pesa za Makaratasi yasiyokuwa na thamani yoyote
6. Mapato yake ni Ngawira, Kharaj, Ushr, Zaka n.k Mapato yake ni Kutoza Raia Ushuru na Kodi (PAYE,VAT,NSSF,NHIF n.k), na Mikopo ya Riba
7. Ni haramu: kurundika mali, ukiritimba katika biashara, riba, bahati nasibu, udanganyifu na uhalifu katika biashara, kujiusisha na biashara za pombe, madawa ya kulevya, madanguro, makampuni ya bima, hisa n.k Ni halali:  Ni haramu: kurundika mali, ukiritimba katika biashara, riba, bahati nasibu, udanganyifu na uhalifu katika biashara, kujiusisha na biashara za pombe, madawa ya kulevya, madanguro, makampuni ya bima, hisa n.k
8. Uchumi hupimwa kwa wepesi wa kukidhi mahitaji msingi ya raia binafsi na mujtamaa Uchumi hupimwa kwa wepesi wa viwanda kuzalisha na mauzo ya bidhaa na huduma
9. Raia thamani yake ni uchajimungu Raia thamani yake ni mchango wake katika uzalishaji wa huduma na bidhaa
10. Mshahara wa Mtu hutegemea manufaa yanayopatikana kutokana na juhudi yake Mshahara wa Mtu hutegemea kiwango cha chini cha matumizi yake ya siku
11. Manufaa ni chochote chenye sifa ya kushibisha mahitaji ya binadamu Manufaa ni chochote chenye kutia faida ima kina sifa ya kushibisha au la mahitaji ya binadamu
12. Utajiri ni mali pamoja na juhudi ya kuizalisha Utajiri ni mali pasi na juhudi ya kuizalisha
13. Raia ni watumwa wa Mwenyezi Mungu (swt) Raia ni watumwa wa wamiliki wa viwanda
14. Pesa ni sarafu ya kubadilishana katika ununuzi wa bidhaa au huduma Pesa ni bidhaa kama bidhaa nyingine yoyote na hivyo inauzwa na kununuliwa

Wakati ni sasa wa kujiunga na ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah itahakikisha kuwa mfumo wa Kiislamu na nidhamu zake zote utatekelezwa kwa ukamilifu ili iwe chanzo cha utulivu na ustawi wa kikweli wa wanadamu. Kinyume na hali ilivyo hivi sasa chini ya mfumo batili wa kisekula wa kikoloni wa kirasilimali kila mmoja yuenda mbio si tajiri si masikini kila mmoja anamvizia mwenziwe amkamue kwa kuwa nidhamu yake ya uchumi imekitwa katika dhana!

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya