Taarifa za Eneo

Utiifu kwa Wamagharibi Unazidisha Madhila kwa Kenya

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikamilisha ziara yake Afrika kwa kuzuru Kenya mnamo 14 Machi 2019 baada ya kuzizuru Ethiopia na Djibouti katika mpango wake wa hivi karibuni wa kuivuta karibu Afrika. Bwana Macron aliahidi ushirikiano mkubwa kwa utawala wa Kenya katika juhudi za kimaendeleo ili kuboresha mazingira na kupambana na misimamo mikali.

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Kenya tungependa kutaja yafuatayo:

Ufaransa ni msimamizi wa Warasilimali Wamagharibi kwa kutumia kisingizo cha ushirikiano wa kimaendeleo, kwa kuwa kambi zake za kijeshi katika nchi kama Djibouti zinajaribu kumakinisha athari za kisiasa katika makoloni yake ya zamani. Ikiwa maarufu kutokana na fikra zake za uhuru wa kugawanya, inakwenda mbio kupigia debe fikra zake ovu za uhuru chini ya bango la diplomasia ambayo ilipelekea Kenya kujumuishwa katika mpango wa Eneo Kipaombele la Ushirikiano (ZSP) na serikali ya Ufaransa mnamo 1999. Huku Macron akiahidi kuboresha uchumi wa mataifa kama Kenya na Pembe ya Afrika ilhali utawala wake una kumbwa na janga kubwa ambalo lilipelekea maandamano ya vurugu kwa wiki tatu mwishoni mwa mwaka jana. Waandamanaji wa “Yellow Vest” wanadai utawala wake uwape afueni ya kifedha kutokana na kuwa idadi kubwa ya maeneo ya watu wanashindwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Ni wazi kuwa ziara ya Macron inalenga kuiwekea Kenya sera ngumu za kiuchumi za kikoloni kama jaribio la kuunusuru uchumi wake ambao unaendelea kusambaratika kiuchumi na kijeshi tokea Vita vya Dunia vya Pili hadi leo.

Ama kuhusu mazingira na mazungumzo ya kusuluhisha changamoto za kimazingira katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) na Kongamano la Sayari Moja, ni porojo tu kwani si kweli kuwa wanataka kusuluhisha changamoto hizi na kuupelekea ulimwengu katika “mbeleni iliyo bora.” Wanafikra wa Kimagharibi na wajuzi wa kimazingira wanakwenda mbio kimakusudi kupambana na athari ya matatizo na sio mzizi wa tatizo. Tunasema kuwa kuharibika kwa mazingira kunatokana na ulafi wa warasilimali ambao wako kuhakikisha wanapata utajiri kwa hali yoyote. Na kwa kuwa nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali imekitwa katika mtizamo wa kimakosa ya kuwa eti tatizo la kiuchumi ni uhaba wa rasilimali na suluhisho lake ni serikali kuhakikisha kuwa wanazidisha uzalishaji ili kuweza kufikia kiwango cha juu zaidi cha Mapato ya Taifa na kuzidisha ukuwaji wa uchumi pasi na kutilia maanani mazingira.

Kuhusiana na matamshi ya Macron kuhusu kupambana na misimamo mikali ya kieneo na kuweka usalama, tungependa kusema kuwa Ufaransa haina hadhi ya kuielekeza Kenya na Afrika kwa ujumla kuhusiana na masuala ya usalama. Jeshi la Ufaransa linajulikana kwa ugaidi na ukandamizaji wake kati ya 1954 na 1962 ambao iliua kinyama takribani wa Algeria milioni 1.5. Walilenga watu jumla na kuangamiza vijiji vyote. Wanajeshi wao etia kutoka katika “taifa lenye ustaarabu” lilifanya ubakaji, mateso na kukata vichwa watu… Fauka ya hayo, wanajeshi wa Ufaransa chini ya pazia ya kuunusuru mpango wa amani Afrika limehusishwa na vurugu moja kwa moja katika sehemu nyingi za Afrika

Kwa kuhitimisha, tunasema kwa kuwa Afrika ni eneo muhimu la kidunia katika mchakato wa Karne ya 21, vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali imekuwa mbinu mpya inayotumika katika kung’ang’ania uporaji wa Afrika. Kuwa mtiifu kwa Wamagharibi itazidisha madhila kwa watu wa Kenya na Afrika jumla. Hivyo basi, tunawalingania wanafikra kujiunga nasi kufanya kazi ya kuleta tena heshima na hadhi kwa watu wa Kenya na Afrika jumla kwa kusimamisha Khilafah ndani ya ardhi ya Waislamu. Ni Khilafah pekee ambayo ina uwezo wa kukatilia mbali mahusiano na wakoloni.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 1440 / 06

Ijumaa, 8 Rajab 1440H /

15/03/2019 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke