Taarifa za Eneo

Waislamu: Waathiriwa/Wahanga wa sera za ubabe na uchu wa Ukoloni wa Kimagharibi.

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

Taarifa kwa vyombo vya Habari
Baada ya siku kumi na mbili za utekwaji wake, msomi maarufu wa Kiislamu  na wakili, Profesa Hassan Nandwa, alipatikana akiwa hai majira ya saa saba usiku Novemba 09 2021 katika msitu ulioko karibu na mji wa Mwingi. Kama visa vingi vya hapo awali, profesa aliamuriwa kutozungumza kabisa masaibu aliyokumbana nayo vyenginevyo atakiona cha mtema kuni! Kulingana na duru za mashirika ya haki za kibinadamu, mwaku huu zaidi ya watu 133 yasemekana ima kuwa wemeuawa au kuchukuliwa na watu hadi mahala pasipojulikana. Tokea mwaka 2007, inakisiwa kwamba zaidi ya watu 1000 wameuwawa au kutojulikana walioko na hatima yao ikibakia kizungu mkuti huku serikali haijaonesha angaa msaada wowote ule.
Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Kenya inakashifu na kulaani kwa ukali matendo haya ya kuhofisha na ya kikatili dhidi ya rai waso na nguvu ya kujitetea yanayofanywa na vyombo vya usalama ambavyo kiasili vinatakikana kulinda haki na usalama wa raia. Kwa uhakika ukiukwaji huu mkubwa wa haki za kibinadamu wa maofisaa wa uslamu ni ishara wazi sifa ya kutojali kwake serikali na kukiuka katiba ya nchi. Watekelezaji wa uhalifu huu bila shaka wanafahamu vyema kwamba hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao kwani wanapata ulinzi mkubwa. Hata hivyo sisi tunafahamu kwa yakini kwamba MwenyeziMungu Swt sio mwenye kughafilika na wanayoyatenda.
Udhalilifu na unyanyasaji huu unaoshuhudiwa leo ni sehemu tu ya maonevu mengi yanayofanyiwa Waislamu kote duniani chini ya kibandiko cha ‘Vita dhidi ya Ugaidi’. Vita hivi vilibuniwa na wamagharibi kama mbinu ya kusukuma malengo na madhumuni yao; Trojan horse ya kikoloni katika kudhibiti oparesheni za usalama wa mataifa ya ulimwengu wa tatu kumakinisha na kuendeleza zaidi ukoloni wao mambo leo. Kiukweli vita hivi vimewafanya waislamu wawe wahanga wa ubabe na uchu wa wakoloni. Ni bayana kwamba vita hivi vinaonesha kufilisika kifikra na kisiasa kwa mfumo wa ubepari na fikra zake za kilebrali.
Mateso haya hayotokoma hadi pale Waislamu warudie faradhi yao walioitupa na kuulingania Uislamu kwa lengo la kuregesha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Raashida kwa njia ya Mtume. Njia hiyo haihusishi lolote lile ispokua kuingia kwenye mvutano wa kifikra na kisiasa.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari
 Hizb ut Tahrir Kenya