Jumla

Wamagharibi wana Wasiwasi na Kurudi kwa Khilafah Ambao Wakati wake Umefika

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila muda unavyo songa ndiyo kusimama kwa Khilafah kunakaribia tena kasi mno! Hii ni kwa sababu sisi Waislamu tunaamini kuwa tuko katika mwisho wa utawala za kidikteta zilizopo duniani zinazoongozwa na Amerika na washirika wake kwa kisingizio cha kupambana na misimamo mikali na ugaidi kwa kutumia mikakati ya kijeshi na kifikra. Maamuzi yao yanatokamana na kwamba kwenda kwao mbio kutahakikisha lengo la kusimamisha Khilafah halitofikiwa. Kwani kurudi kwa Khilafah ni kurudi kwa enzi ya dhahabu chini ya hadhara ya Kiislamu ambao utasuluhisha matatizo yote yaliyo sababishwa na hadhara ovu ya Kimagharibi.  Mbinu zao zinatokamana na kumbukumbu walizonazo kuhusiana na Khilafah ambazo zimebakia katika mabongo ya wasomi Wamagharibi hususan wanahistoria wao. Yafuatayo ni baadhi ya maandishi ya wanahistoria wao kuhusiana na Khilafah:

Mwanahistoria, Joseph Hilaire Pierre René Belloc:

“Mamilioni ya watu wa zama hizi wa hadhara nyeupe –yaani hadhara ya Ulaya na Amerika- wamesahau yote kuhusiana na Uislamu. Hawakuwahi kupambana nao. Wanaona ni jambo dogo kuuwacha ukiozelea mbali na kwa njia hiyo wanauona kama dini ya kigeni ambayo haiwahusu wao. Na kwa ukweli ndio adui mwenye nguvu na wakudumu ambaye hadhara yetu imekuwa naye na ambaye wakati wowote anaweza kuwa tishio kubwa hivi karibuni kama ilivyokuwa hapo zamani…Nguvu jumla za kiroho za Uislamu zipo hadi leo ndani  ya watu wa Syria na Anatolia, milimani mwa Mashariki ya Asia, Arabia, Misri na Afrika Kaskazini. Matunda ya mwisho ya uadui huu ni kurudi tena kwa mara ya pili utawala wa Kiislamu, inaweza kucheleweshwa…lakini sioni kwamba inawezekana kucheleweshwa milele.”

Mwanahistoria, Bernard Lewis:

“Wilaya zote isipokuwa za mashariki zilizomo katika utawala wa Uislamu zilitekwa kutoka kwa watawala Wakristo… Afrika Kaskazini, Misri, Syria, Iraq iliyo tawaliwa na Fursi zilikuwa nchi za Kikristo ambao Ukristo ulikuwa ni wa zamani na umekita mizizi zaidi kuliko ndani ya Ulaya. Kutekwa kwao ilikuwa hasara kubwa na ikapelekea kuhisi na kuzidisha vitisho kwamba hatima hiyo itaikumba Ulaya yote.”

Kauli hizo zinadhihirisha kuwa Wamagharibi wasomi ima walio fariki au hai kwa pamoja wanahofia siku ambayo hadhara yao iliyofeli ya Kimagharibi itakapoondoshwa na hadhara ya Kiislamu chini ya Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah itatawala dunia kwa kupeana utulivu, maendeleo na ustawi kwa binadamu pasina kujali tofauti za dini, rangi, kabila au cheo. Khilafah itakuwa ndiye mlinzi na ngao ya kweli kwa wanadamu kama ilivyo shuhudiwa kwa takribani Karne 13 za uongozi wake. Kama Waislamu ambao tuna ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na bishara kutoka kwa Mtume (saw); lazima tuzidishe juhudi usiku na mchana kwa kufanya kazi ya kurudisha Khilafah Rashidah, Mlinzi Wetu, Ngao Yetu.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Makala Na.38: Ijumaa, 22 Rajab 1440 | 2019/03/29