Habari na Maoni

“Watoto kwa Pesa” ni Mfano Mwengine wa Faida za Kirasilimali Zinazothaminiwa Kuliko Maadili ya Kiutu

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Mnamo 8 Julai gazeti la New York Times liliripoti juu ya mpango mpya zaidi wa kibiashara wa Raisi wa Amerika uliolenga kuyawekea kizuizi maazimio ya Umoja wa Mataifa ya kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama katika ngazi ya kimataifa, akiyataja kuwa mbinu bora zaidi ya kukuza afya ya watoto wachanga. Ujumbe wa Amerika, unaokumbatia maslahi ya watengezaji maziwa ya unga ya watoto, ulijaribu “kupinga azimio hilo kwa kuiondoa lugha inayotoa wito kwa serikali “kulinda, kupigia debe na kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama” huku ukipigia debe bidhaa na mbinu za lishe zilizothibitisha kuwa na athari mbaya kwa afya na ukuaji wa watoto wachanga.

Maoni:

Unyama wa hali ya juu wa mfumo wa kirasilimali umejitokeza wazi wazi katika mfano huu makhsusi wa kisiasa ambapo Amerika chini ya Raisi Trump kupitia utoaji maagizo ya moja kwa moja, inatafuta kuweka adhabu za kiuchumi na shinikizo la kidiplomasia juu ya nchi zile ziliounga mkono mswada wa unyonyeshaji maziwa ya mama. Ecuador ndio nchi ya kwanza iliyoingia katikati ya mipaka ya faida ya kikosi cha kibiashara cha Amerika huku Washington ikisema wazi wazi kuwa itatoa “hatua za kiadhabu za kibiashara na kuondoa msaada wake muhimu wa kijeshi” natija yake serikali ya Ecuador ilitishika na kwa haraka ikabadilisha msimamo wake na kufuata agizo la Amerika. Mbinu hii ya utumiaji pazia ya demokrasia na huku ikitumia hatua kali zaidi za kiimla dhidi ya umbile lolote linalokiuka maslahi yake ndio mkakati asili wa mataifa yote ya kirasilimali yaliyoko. Kama natija yake daima tutarajie kuwa thamani ya maisha, afya ya binadamu na manufaa ya watu (hata wale walio katika hali ya udhaifu kama wazee na watoto wachanga) daima watatolewa kafara juu ya jukwaa la mapato ya kifedha na nguvu ya kisiasa, kwani haya ndio ‘miungu’ inayoabudiwa juu ya mambo mengine yote. Nchi zilizosibiwa na ghadhabu za Amerika ziliweka wazi mapendekezo yao lakini “zikaomba kutojitambulisha peupe kwa sababu ya kuhofia kushambuliwa na Amerika.”

Mbinu hizi hizi ambazo mataifa ya kidemokrasia huzikashifu mataifa mengine yanayoitwa mataifa ambayo hajastaarabika ya ulimwengu wa tatu, ndizo hizi hizi zinazotumika mara kwa mara ili kupata manufaa yanayotumikia maslahi ya kitaifa. Unafiki huu unadhihirika kutokana na kuanzishwa kwa urasilimali na licha ya madai ya mabadiliko, daima zitabakia kuwa kitovu cha yale matunda ya urasilimali kwa wanadamu.

Tunapo tofautisha haya na sera adilifu za kiutu za Kiislamu tutaona tofauti kubwa katika nidhamu mbili hizi za kimaisha na jinsi gani zinavyoafikiana na maumbile ya wanadamu na kuinua kiwango chao cha maendeleo. Uislamu haukubali utawala wa mabwenyenye wachache kwa gharama ya ugandamizaji wa wengine ulimwenguni. Eneo lolote lililokubali kuishi chini ya utawala wa Khilafah daima lilifanywa kuwa bora katika kila nyanja zake za kijamii na kisiasa. Hata baada ya Uislamu kuondoka kama muundo wa kisiasa, watu walibakia kuwa Waislamu na athari nzuri ya Uislamu imebakia baada ya karne kadhaa ikiwa ni mfano wa kufurahikiwa na kutafutwa tena kwa mara nyengine.

Ajenda za kibepari na za kikoloni za Ulaya na Amerika hazina urithi kama huo kwani taifa lolote lililokumbana na nidhamu yake ya utawala liliambulia kuteseka mateso mabaya mno ya ukiukwaji haki za kibinadamu huku ardhi zake zikikamuliwa na kufujwa rasilimali zake. Siku za nyuma na hadi leo, utumizi wa kimakusudi wa vita na baa la njaa hutumika kama silaha za kimakusudi za kudhibiti ili mataifa ya kirasilimali yadumishe udhibiti huu juu ya wengine kwa vitisho na nguvu, sio kupitia watu wenyewe kuyaona kwa khiari mafanikio ya kimaadili na kijamii ya mfumo huu wa kimaisha.

Tunamuomba Allah (swt) kwa mara nyengine tena airudishe nidhamu hii ya utawala nzuri iso kifani katika biladi za Waislamu ili kule kusakamwa na kupaliwa kutokanako na nidhamu ya uhuru ya kidemokrasia na sera za kirasilimali ziondolewe uwepo wake ili kuruhusu ukombozi unaohitajiwa na ulimwengu kutokana na udhibiti muovu wa sheria fisidifu zilizotungwa na wanadamu.

Allah (swt) ameusifu utawala wa Uislamu kuwa safi na adilifu kwani unatoka kwa Muumba wa watu na hauhudumii maslahi mengineyo ya kibinafsi;

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّهَ﴾ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا﴿

“Enyi mlioa amini! Kuweni wenye kusimamia uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Mkiupotoa au mkijitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.” [An-Nisaa: 135]

Kutokana na hili tunaweza kuona kuwa kurudi kwa Dola ya Kiislamu pekee, Khilafah katika njia ya Mtume (saw) ndiko kutakako hudumia maslahi bora kwa watu wote vijana na wazee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad